- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Kwa kuzingatia matokeo ya mitihani ya taifa ya wanafunzi wa kidato cha nne kwa miaka mitatatu mfululizo, hali ya kitaaluma katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara inaridhisha.” Alisema Kaimu Afisaelimu idara ya sekondari ndugu Marton James akiwa ofisini kwake.
Afisaelimu James amesema ufaulu umeongezeka kwani kuanzia mwaka 2015 hadi 2017, ufaulu wa wanafunzi umeogezeka na kufikia wastani wa 79%, ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2015, ambapo wanafunzi wa kidato cha nne walifaulu kwa wastani wa 67% pekee.
“Kutokana na matokeo hayo Halmashauri yetu imefanikiwa kushika nafasi zifuatazo kimkoa mwaka 2015 ilikuwa ya nne (04), mwaka 2016 ilikuwa ya nne (04) ambapo mwaka 2017 ilikuwa ya tatu (03) kati ya Halmashauri nane (08) za mkoa wa Kagera.” Alisema afisaelimu huyo.
Aidha, amesema mbali na kufanya vizuri katika mithani ya kitaifa; kila Tarafa ina shule ya kidato cha tano na cha sita na kila kata inamiliki shule ya sekondari, isipokuwa kata moja ya Nyamagoma aliyoitaja kuwa ni mpya.
Akijibu swali kwa nini mafanikio hayo, alisema yanafuatia juhudi mbalimbali alizozitaja kuwa ni ufuatiliaji na usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule za sekondari.
Hata hivyo amesema kuwa utoro, maadalizi hafifu ya ufundishaji, umbali mrefu wa makazi ya wanafunzi na walimu, ni baadhi ya changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao.
Afisaelimu huyo ameongeza kuwa wanakabiliana na changamoto hizo kwa kutoa hamasa kwa wazazi na wanafunzi ili watambue umuhimu wa elimu, wakuu wa shule wameelekezwa kusimamia mahudhurio ya wanafunzi ili kudhibiti utoro wa rejareja, pamoja na kuwatuza wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kupitia idara ya elimu sekondari inasimamia taaluma katika shule za sekondari 29, amabapo shule 23 zinamilikiwa na serikali na shule sita zinamilikiwa na sekta binafsi. Pia inamiliki shule moja pekee yenye kidato cha tano na cha sita.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa