- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Chumba kipya cha darasa kimezinduliwa katika shule ya msingi Mumiterama kata ya Nyamiaga na mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Diwani wa kata ya Nyamiaga mh. Julius Ernest. Chumba hicho kimewezeshwa na mradi wa Programme for Result (P4R) ambao ulichangia kiasi cha shilingi milioni 6. Huu ni mradi ambao unahusisha halmashauri kupitia idara ya elimu kupokea pesa kulingana na matokeo. Katika hafla hiyo wazazi wa wanafunzi na wanakijiji pia walialikwa kuhudhuria. Kutokana na kukidhi vigezo vya P4R halmashauri ya wilaya ya Ngara ilipokea kiasi cha shilingi milioni 384.7 na katika pesa hizo ndipo shule ya msingi Mumiterama ilipatiwa kiasi cha shilingi milioni 6 ili kiweze kumalizia chumba cha darasa
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa