- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Hospitali ya Wilaya ya Ngara, iliyopo kata ya Mbuba imewekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023, Ndg. Abdalla Shaib Kaim baada ya kutembelea na kukagua shughuli za ujenzi zinazoendelea katika mradi huo
Akizungumza na wananchi, Ndg. Abdalla Shaib Kaim ameeleza kuwa kwa fedha ambazo hadi sasa zimetolewa na Serikali Kuu, kazi kubwa ya ujenzi imefanyika kwa ubora, viwango na inadhirisha. Na kutoa pongezi kwa viongozi na wataalam
“Baada ya kupata maelezo nakufanya ukaguzi wa kina, tumejiridhisha hakuna shaka lolote kwenye matumizi ya fedha.Hatua ya ujenzi ambao mradi umefika ubora na viwango vimezingatiwa. Lengo ni usimamizi wa mradi ukamilike kwa wakati wananchi waendelee kupata huduma kama ilivyo nia ya dhati ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea wananchi maendeleo,” ameeleza Ndg. Abdalla Shaib
Akiwa katika mradi wa vijana waliowezeshwa kiuchumi na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkopo wa asilimia 10 kwa Wanawake, Vijana na Waatu Wenye Ulemavu na kuanzisha shamba la parachichi na kitalu cha miche ya mizinga ya nyuki amewapongeza vijana hao kwakuwa na shamba zuri, lenye uhai na bora linalowawezesha kuinua hali yao ya kiuchumi
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi, akiupokea mwenge wa Uhuru katika viwanja vya soko la Benaco ukitokea Wilaya ya Karagwe ameeleza kuwa kwa Wilaya ya Ngara Mwenge wa Uhuru utatembelea, utakagua, utaweka mawe ya msingi na kuzindua jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Tsh. bilioni 1.7
Miradi hiyo ni vyumba vitano vya madarasa shule ya msingi Rulenge vyenye thamani ya Tsh. milioni 100, barabara ya Rulenge kwa kiwango cha lami km 0.476 yenye thamani ya Tsh. 142.2 na ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngara iliyogharimu Tsh. milioni 150.
Aidha mradi wa uboreshaji huduma ya maji Ngara Mjini umegharimu Tsh. milioni 234.7 na mradi wa Vijana shamba la Parachichi,kitalu cha miche ya mizinga ya nyuki wanufaika wa mkopo wa Halmashauri waliowezeshwa Tsh. milioni 130.
Mhe. Kanali Kahabi amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha za miradi ili kutekeleza maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Ngara. Pi amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuushangilia mwenge wa Uhuru mwaka 2023 katika maeneo yote mwenge wa Uhuru ulipopita.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa