- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mganga Mfawidhi wa Kitu cha Afya cha Murusagamba Dr. Godian Beyanga, amesema majengo yanayojengwa yakikamilika yatawapunguzia adha wananchi ya kusafiri umbali mrefu, kufuata huduma katika Hospitali za Rulenga, Murugwanza na Nyamiaga Ngara.
Mganga Beyanga amemwambia hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama Mei 24, 2018, alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la kuwapokea wagonjwa (OPD), jengo la upasuaji (Theater), wodi ya mama na mtoto (IPD), nyumba ya mganga na sehemu ya kufuria nguo.
Amesema kwamba kati ya shilingi milioni 400 walizopokea; shilingi milioni 202,000,000.00 zimetumika hadi Mei 24, 2018, shilingi milioni 198,000,000.00 zilikuwa hazijatumika, ambapo majengo yote yamefikia hatua nzuri.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bahama, amesema amelizika na kasi ya ujenzi wa majengo hayo, na kuwataka kuhakikisha yanakamilika kwa wakati kwani lengo la majengo hayo ni kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata huduma ya matibabu mbali na makazi yao.
Kituo cha Afya cha Murusagamba kinatoa huduma kwa wananchi wanaotoka katika kata tatu, ambazo ni Murusagamba, Muganza na Nyamagoma kadiri ya Dr. Beyanga kituo hivho cha afya kihudumia wastani wa wagonjwa 120 kwa siku.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa