- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Kahawa imezuiliwa kununuliwa na mtu wa kawaida; mkulima anatakiwa aivune, na aiuze kahawa yake kwa chama cha ushirika; ukinunua kahawa kwa mkulima tukakujua kazi yetu ni kukufilisi.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama.
Mkurugenzi huyo alikuwa akiongea na wanakijiji wa Chivu, kata ya Kirushya Julai 30, 2018, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, kwamba Ndugu Rafaeli Festo Nfizi anavuna kahawa ya wakulima kinyume na utaratibu uliowekwa na serikali.
Ndugu Rafaeli alikuwa amekwisha vuna gunia zipatazo kumi na moja kwa shilingi 40,000/= tu, kitendo ambacho Mkurugenzi Mtendaji alikitaja kuwa ni cha kinyonyaji na cha kuwanyanyasa wananchi wa kawaida.
Baada ya kupata taarifa kwamba Mkurugenzi na timu yake, wanakwenda nyumbani kwa Ndugu Rafaeli, alikimbia; timu ilikuta gunia kumi na moja za kahawa alizokuwa amevuna kwa wakulima.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Chivu, amesema chama cha ushirika cha Ngara Farmers Corporative mwaka 2018, kimepewa dhamana ya kukusanya kahawa yote ya wakulima wilayani Ngara.
“Kwa sababu Ndugu Rafael amekiuka utaratibu uliowekwa na serikali na kwa makusudi akamua kuendelea kufanya ufisadi wake, tutamfilisi kahawa yote, na itakuwa mali ya serikali.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bahama.
Ndugu Bahama amewaambia wananchi hao kufikisha ujumbe huo kwa wengine kwamba Kama kuna mtu alinunua kahawa ikiwa shambani asubiri mkulima aiuze, ili baada ya kuuza amlipe mlangunzi pesa yake; lakini mlanguzi hana ruhusa ya kuvuna kahawa ya mkulima.
Wakati huo huo, katika kjiji cha Mwivuza kata ya Kirushya timu hiyo ya Mkurugenzi ilimkamata Mwenyekiti wa Kitongoji cha Murugalama ‘A’ kijiji cha Mwivuza kata ya Kirushya, Ndugu Alani Jason, akituhumiwa kupokea kiasi cha shilingi 30,000/= kutoka kwa Sifa ili amruhusu mlanguzi kuvuna kahawa kwa wakulima.
Timu ilifanikiwa kukamata gunia nane toka kwa mkulima aliyekuwa ametunza kahawa za mlanguzi aliyejulikana kwa jina moja la Sifa wa kitongoji cha Lunzenze kata ya Ntobeye, nakufikisha jumla ya gunia zilizokamatwa 19.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Halmashauri ametoa wito kwamba waende wawaambie na wengine wasijaribu kuchukua kahawa ya mtu na wala wasijaribu kununua kahawa kwa mkulima yoyote.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa