- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ukosefu wa maadili mema kiutendaji, misingi ya utawala bora pamoja na ikiukaji wa sheria kwa baadhi ya viongozi katika mataifa mbalimbali Afrika, ni baadhi ya vikwazo vinavyohatarisha haki za binadamu na kukosekana kwa amani ya kudumu barani humu.
Mkuu wa shirika la Mapadre wa Yesu (Jesuit Fathers) Afrika mashariki, Padre Joseph Oduor Afulo, amebainisha hayo Januari 22, 2018, baada ya kutembelea wilaya ya Ngara mkoani Kagera, kuwahamasisha mapadre waliojiunga na shirika hilo, ili baadae waweze kudumisha amani na utulivu watakapoanza kazi za kiroho.
Shirika la mapadre hao ukanda wa Afrika Mashariki unajumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudani kusini na kaskazini, ambapo kazi yao kubwa ni husimamia miradi ya elimu, Afya, huduma kwa wakimbizi (Jesuit Refugees Service), amani na maridhiano na kuhamasisha haki za binadamu barani Afrika.
Padre Afulo amesema bara la Afrika limepoteza amani na utulivu kutokana na viongozi wenye dhamana kutofuata misingi ya utawala bora, kukuza demokrasia lakini pia baadhi yao hawatumii kanuni na sheria kulinda maslahi ya mataifa wanayoyaongoza baada ya kupatiwa dhamana na wananchi au mamalaka zinazohusika.
"Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, wanaokiuka haki za binadamu wanakosa malezi kifamilia, kutokuwa na adabu na utii na kukiuka misingi ya kiroho, ndiyo hao hao katika makanisa na misikiti licha ya kuonekana watu wema mchana, lakini usiku wanafanya kinyume" Amesema Afulo
Alisema mataifa mengi yamekosa mwelekeo wa amani na utulivu yemejaa mateso, kuwepo changamoto ya vurugu za kisiasa, kiuchumi na kijamii lakini pia utendaji wa viongozi wa kisiasa umekuwa wa kujichukulia maamuzi badala ya kufuata waliyotumwa na waliowachagua.
Ameshauri viongozi duniani hasa wenye mamlaka wawe wakweli katika kutamka na kutenda, ili kudumisha amani badala ya kusababisha machafuko, vita na dhuluma na kila mmoja aguswe na tatizo la mwingine kwa kuanzia ngazi ya familia ili kuwepo usalama kila taifa.
Mesikitishwa na mifumo ya elimu inayotolewa hivi sasa kwa wanafunzi kwamba haihamasishi viongozi mbalimbali duniani kuwajenga wananchi kujitegemea, matokeo yake wanasababisha matabaka, kwani watoto wa viongozi husomea katika shule zenye gharama kubwa; huku wakiwa tegemezi kiakili.
Kabla ya uhuru wanafunzi walijifunza elimu ya kujitegemea, kwa sasa wanalundikiwa masomo mengi, wakijifunza kujibu mitihani kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu, na kila anayepata nafasi, anakuwa fisadi kwa kila mbinu, ili kujinufaisha.
"Inafaa wazazi kuwalea watoto kwa nidhamu maana aja ya mja hunena; lakini kutolewe elimu ya kujitegemea, kuepuka kupata viongozi na watendaji mafisadi, wala rushwa na wenye kukiuka haki za wengine" Aliongeza.
Akiwa wilayani Ngara aliwapongeza wandishi wa habari wa Radio Kwizera, kwa utendaji kazi wao katika kuhabarisha jamii na kuhimiza utawala bora, upatikanaji wa haki za binadamu na kwamba lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kujua hali ya majesuit kwa huduma wanazofanya hapa nchini.
Awali akiwa na wenyeji wake wilayani Ngara Padri Fredrick Meela, alisema katika kusimamia majukumu na utendaji wa shirika hilo, kwa wilaya ya Ngara na wilaya zinazounda mkoa wa Kigoma, wananchi wanapata huduma za kuwajenga kiroho na kuwapa matumaini.
Alisema upashanaji wa habari hupitia njia ya Radio Kwizera kwa kuweka wanahabari maeneo mbalimbali, zikiwemom kambi za wakimbizi mkoani Kigoma; lakini hata maeneo mengine kwa baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa Viktoria.
Amesema pia mapadre hao wanasimamia elimu maeneo mbalimbali nchini kama vile Loyola iliyoko Mabibo jijini Dar es Salaam, St Peter Claver ya mkoani Dodoma zikiwemo shule za msingi lakini pia shule hizo hutoa huduma za afya kwa ajili ya wanafunzi na walimu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa