- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mradi wa Umeme wa Maji wa Regional Rusumo Falls Hydro-electric Project (RRFHP), utakaokuwa na uwezo wa kutoa MW 80 za umeme hadi unakamilika, utagharimu dola za kimarekani 471.
Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kwa waandishi wa habari, iliyotolewa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati wa Tanzania Mh. Dr. Medard Kalemani, Waziri wa Miundombinu wa Rwanda Mh. Balozi Claver Gatete, pamoja na Waziri wa Nishati wa Rwanda Mh. Kamayirese Germaine June 09, 2018 katika eneo la mradi huo wa Umeme.
Kadiri ya taarifa hiyo mradi wa RRFHP utakapokamilika utakuza uchumi wa nchi hizo tatu katika shughuli mbalimbali kama vile kuzalisha umeme nafuu na kutunza mazingira kwani utapunguza gharama za kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme.
Mradi huo utazinufaisha nchi tatu ambazo ni Tanzania, Burundi na Rwanda, ambapo kila moja itapata mgawo wa umeme wa MW 26.7 kati ya MW 80 zitakazozalishwa na mradi huo; kadiri ya Waziri Dr. Kalemani kiasi hicho cha umeme ni muhimu kwa Tanzania.
“Sisi Tanzania tunauhitaji umeme huo zaidi, ili kuimarisha sekta ya uchumi wetu kama, ambavyo tunasema kujenga uchumi wa viwanda; ndiyo maana tunaukagua ili tuweke msukumo ukamilike haraka.” Alisema Mh. Dr. Kalemani.
Pamoja na nchi tatu kunufaika kwa MW 80 za umeme, bado wananchi wanaouzunguka mradi huo, watanufaika na miradi ya maendeleo, ambayo ni ya afya, elimu na kilimo, itakayofadhiriwa na mradi wa RRFHP.
Maeneo yatakayopewa kipaumbele katika miradi ya wananchi ni Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Tanzania, mikoa ya Busoni na Giteranyi nchini Burundi pamoja na wilaya ya za Ngoma na Kirehe nchini Rwanda.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa