- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mratibu wa TASAF kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri tayari wameanza kusimamia utekelezaji wa miradi ya kutoa ajira za muda (PWP) kwa walengwa wa mpango wa TASAF III. Miradi hii ni ya hiari na sio ya lazima na inatakiwa kukamilika ndani ya siku sitini. Walengwa wamepewa vifaa kwa ajili ya kuhakikisha miradi hiyo inakamilika na tayari timu ya ukaguzi wa vifaa imeshateuliwa na Mkurugenzi ikiongozwa na Afisa Ugavi ndg. Koelet Manyama ili iweze kukagua vifaa ambavyo wazabuni wamevisambaza katika vijiji husika kama vimekamilika ili kuwawezesha walengwa kutekeleza miradi hiyo. Aidha timu ya wataalam hufika kwenye maeneo husika na kutoa ushauri wa namna miradi hiyo inavyopaswa kutekelezwa na kusimamia ili kuhakikisha yale wanayoyashauri yanafanyiwa kazi. Kwa mfano kwenye ulimaji na uchongaji wa barabara, mhandisi wa ujenzi ndiye anayehusika na kutoa ushauri wa vifaa vipi vinunuliwe na si hivyo tuu huwaelekeza walengwa nini cha kufanya wakati wakiwa kwenye eneo la kazi. Baadhi ya miradi iliyoibuliwa na walengwa ni ujenzi wa malambo ya kuhifadhia maji ya kunyweshea mifugo, ulimaji na uchongaji wa barabara kwa kutumia mikono, ujenzi wa vyanzo vya maji na uapandaji wa miti.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa