- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo Mhashamu Baba Darlington Misago Bendankeha Askofu Dayosisi ya kagera amezingua Jengo la famasi na Kozi ya famasi liliojengwa kutokana na makusanyo ya ada ya chuo murgwanza institute of Health and Allied sciences (MURIHAS ) Jengo hilo lenye zaidi ya thamani ya Tsh Milioni 126,056,000/=
Baada ya kukata utepe na kuzindua jengo la maabara ya famasi Mhashamu Baba Askofu aliongoza Ibada Maalum.
Ibada Maalum ilipomalizika zilianza sherehe za uzinduzi wa Kozi ya famasi, Jengo la maabara ya famasi na kuwakaribisha wanachuo wapya.
Ibada na sherehe hizo zilifanyika viwanja vya chuo cha (Murgwanza Institute of health and Allied sciences) Ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe Ndaisaba George Ruhoro aliyewakilishwa na Ndg Stivine Mabengas. Mratibu wa shughuli za Mbunge Ndg Mathias Mugatha, katibu wa Mbunge Ndg Benedicto , pia viongozi mbalimbali walishiriki ambao ni Mhashamu Baba Askofu ,Vical General Elis Ikambuza , wachungaji Anglican, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Hakimu mkazi Wilaya Mhe kanavalo,Waheshimiwa Madiwani Ngara Mjini, Murukulazo, Ntobeye, Mfamasia Wilaya, Afisa ustawi Wilaya, Mgaga mkuu Wilaya,vingozi Toka Hospital Murgwanza Mganga mkuu, hospitali Murgwanza, katibu hospital Murgwanza,viongozi Toka Dayosisi ya kagera, wageni Toka UK, wakufunzi chuo,Mwalimu mkuu Napsi na wanahabari.
Aidha Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Ngara alitoa Tsh M 1, mifuko 150 ya saruji, mifuko 2 ya Michele Kwa wanachuo, ambapo viongozi waliokuwepo katika hafla hiyo meneja NMB alitoa mifuko 10 ya saruji, meneja CRDB Alitoa TShs laki 4 zitakazowekwa akaunti ya chuo, Mhe Diwani mukiza Byamungu alitoa mifuko 10 ya saruji, Mkurugenzi Ngara famasi alitoa Tsh 240,000 za mifuko 10, Eng aliyefuatana na Mwakilishi Mbunge alitoa mifuko 10, pia kikundi Cha kwaya kilipewa na Mwakilishi Mbunge Tsh 200,000. Mhe Diwani Ngara Mjini aliahidi Tsh 100,000 Mwakilishi wa Mbunge pia atatoa bati 50, computer 2 na kinanda Kwa ajili ya chuo hicho.
Mhashamu Baba Askofu Darlington Misago Bendankeha alimshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Ngara Kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
Pia Mhashamu Baba Askofu alimshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia suruhu Hassan.
Aidha mkuu wa chuo Ndg Ilakiza Gashaza alisema kozi zilizopo ni :
1.Diploma in Nursing and Midwifery.
2.Diploma in pharmaceutical Sciences.
3.Diploma in social work
Mkuu wa chuo cha Murgwanza Institute of Health and Allied sciences akitoa maelezo mafupi ya jengo la maabara ya famasi.
Mhashamu Baba Askofu Darlington Misago Bendankeha Askofu Dayosisi ya kagera akiwa katika picha za pamoja na Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Ngara Ndaisaba G Ruhoro Ndg Stivin mabenga na viongozi Mbalimbali.
Viongozi mbalimbali katika hafla.
Wakitembelea jengo jipya la maabara ya famasi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa