- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoani Kagera waipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kuchukua maamuzi yanayolenga kuwainua wananchi, ili wafaidike na raslimali za nchi yao.
Viongozi hao wa Dini wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ofisini kwake Januari 16, 2019, walimpongeza Rais John Pombe Magufuli, kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini na yenye manufaa kwa umma.
Wakiitaja miradi hiyo kuwa ni ununuzi wa ndege, ujenzi wa Reli ya Kisasa na ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge pamoja na miradi mingine mingi ya maendeleo ya wananchi.
Pia, akiongea kwa niaba yao Askofu wa Jimbo Katoriki la Bukoba, Askofu Msaidizi Methodius Kilaini, alisema wanaipongeza serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli, kwa kudumisha amani, utulivu, mshikamano na kutekeleza miradi inayolenga maslahi ya wananchi.
Viongozi hao waliahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya mkoa katika kudumisha amani na utulivu, ili kudumisha mshikamano kama ilivyo desturi yao na kuhamasisha wananchi kuchapa kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa mkoa kama jina la Mwaka 2019 kwa lugha ya Kihaya linavyohimiza kuwa kila mmoja atakula kwa jasho lake “Biluga Omumpiita”.
Naye, Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti aliwahakikishia Viongozi hao wa Dini, kuwa yeye Binafsi kama Mkuu wa Mkoa wa Kagera pamoja na Serikali ya Mkoa, wataendelea kushirikiana nao, kwani wao ndiyo nguzo kuu ya amani katika mkoa, lakini pia nguzo kuu ya maadili hasa kwa kuiunganisha Serikali na wananchi wake.
“Sisi Serikali tutaendelea kushirikiana na nyinyi kama ilivyo desturi ya Mkoa wetu wa Kagera, na tunawategemea sana katika kuhakikisha mkoa wetu unaendelea kudumisha amani na utulivu, kwani mnapokutana na waamini wenu mkahubiri amani, utulivu na kufanyakazi kwa bidii; sisi kwetu kazi inakuwa ndogo.” Alisistiza Mhe. Gaguti
Viongozi wa Dini waliokutana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoriki la Bukoba Method Kilaini, Sheikh wa Mkoa wa Kagera Aruna Kichwabuta pamoja na Askofu Dkt. Abedinergo Keshomshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kasikazini Magharibi.
Mkuu wa Mkoa alitoa rai kuwa Mkoa wa Kagera ukiongozwa na Kaulimbiu ya “Kazi, Amani na Maendeleo” umejipanga kwa mwaka huu wa 2019, kuwa ni mwaka wa kazi, pia ni mwaka wa wananchi wote hasa wanaojihusisha na biashara ya aina yoyote kulipa kodi, ili kuhakikisha Kagera inarudi kwenye enzi zake za uchumi imara.
Na Sylvester Raphael
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa