- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe. Kanali Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Ndg. Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Ngara pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama.
Wamefanya ziara ya ukaguzi ujenzi wa soko la Kahaza kata ya Rusumo, wamebaini kwamba ujenzi unasuasua kutokana na mkandarasi kuwa na kasi ndogo ya ujenzi, vifaa kidogo vya ujenzi na Mafundi na vibarua wachache.
Mhe Mkuu wa wilaya amechukua hatua ya kuongeza vibarua kutoka 47 Hadi 88 na Mkandarasi atachukuliwa hatua.
Ujenzi wa soko hili umetengewa bajeti ya TSH 2,517,833,000 na Hadi sasa mkandarasi amepewa Tsh. 377,000,000 na bado anasuasua.
"Tutaendelea kuwa wakali sana hatuwezi kukubali pesa anazotoa mheshimiwa Rais wa JMT, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambazo zinaletwa kuhudumia wananchi zichezewe" amesema Mhe Mkuu wa Wilaya.
Mhe Kanali Mathias Kahabi Mkuu wa Wilaya akiwa na Ndg.Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, pia kamati ya Usalama pamoja na mafundi.
Ujenzi wa soko la KAHAZA kata ya Rusumo Wilayani Ngara.
Ujenzi wa soko la KAHAZA linalojengwa Rusumo Wilayani Ngara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa