- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Kuendeleza Biashara na Masoko Ndugu Christopher Chiza, amewaambia wafanyabiashara wa kata ya Rusumo katika Halamashauri ya Wilaya ya Ngara, kwmaba wawe wavumilivu wakati serikali inatafuta suluhisho ya matatizo yao.
Ndugu Chiza ameyasema hayo, wakati alipokutana na wafayabiashara hao Katani Rusumo Aprili 13, 2018, kwamba matatizo yao wameyasikia na kwamba watayawakilisha kwa wahusika, ili ufumbuzi upatikane.
“Sisi hatuna majawabu ya moja kwa moja kwani mnayotuambia yanahusu nchi zetu mbili, lakini tumeyasikia na tutayapeleka kunakohusika na majawabu yatapatikana.” Alisema ndugu Chiza.
Wafanyabiashara hao wamezitaja kero wanazozipata kuwa ni pamoja na kutozwa ushuru mkubwa, kuzuiwa mizigo yao kwa madai kuwa haina vifunganishio, pamoja na usumbufu katika baadhi ya beria hapa nchini.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Biashara katika mamlaka hiyo, ndugu Fidelis B. Mugenyi amesema baadhi ya matatizo hayo, yanawahusu wasimamizi wa ofisi za udhibiti wa mapato, wakati mengine yanawahusu wafanyabiashara wenyewe.
Amesema kwamba kamati za biashara za mpakani, zinajitahidi kuyatatua baadhi,ya matatizo, na mengine inabidi yapelekwe kwenye ngazi za juu kwa ufumbuzi zaidi.
Amewataka kuwa karibu na Mamlaka ya Kuendeleza Biashara na Masoko, ambacho ni chombo cha taifa cha kutatua changamoto zao kwa kuzipeleka kwa taasisi au chombo husika.
Wajumbe hao, kutoka Mamlaka ya kuendeleza Biashara na Masoko nchini, wamemaliza ziara yao katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Kuedelea na ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa