- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakulima wa kahawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuvuna kahawa yote iliyoko mashambani, na kuhakikisha inauzwa katika Chama cha Ushirika cha Ngara Farmers Cooperative.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, ametoa agizo hilo ofisini kwake Julai 23, 2018, kufuatia wakulima kushindwa kuvuna kahawa kwa madai mbalimbali.
“Wakulima wanashindwa kuvuna kahawa kwa sababu baadhi yao walishauza mashamba ya kahawa kwa walanguzi; kwa kuogopa agizo la serikali la kuzuia ulanguzi, wakulima waliouza kahawa wanaogopa kuvuna kahawa, na walanguzi wanaogapa kudai kahawa hiyo.” Alisema Ndugu Bahama.
Wakulima wengi wametunza kahawa hiyo mashambani matokeo yake; kahawa hiyo inadondoka chini na kuharibika pamoja na kupoteza ubora wake; huku akiwaagiza wakulima hao kuhakikisha kahawa hiyo imevunwa na kuuzwa.
Wakulima wa kahawa wa vijiji vya Chivu na Kirushya wakiongelea sababu za kutovuna kahawa kwa wakati walidai kwamba hawana vifaa vya kuanikia kahawa wanayoivuna kwani waliabiwa kahawa isiwe na uchafu.
Wengine wakasema kuwa kuuza kahawa na kulipwa fedha hiyo kwa njia ya mtandao au line ya simu kwao ni tatizo, kwani waliosajiliwa na Benki ya CRDB ni wachahche na baadhi yao walisajiliwa kwa line za ndugu zao.
“Jambo la fedha ni gumu sana kitendo cha kutusajili kutumia line ya mtoto au ndugu litasababisha wachache wetu kupoteza fedha, kwani fedha haina uaminifu.” Alisema mkulima mmojawapo ambaye akutaka jina lake litajwe.
Wakulima hao wameomba chama cha ushirika kununua kahawa hiyo haraka, kwa madai kwamba wanashida na fedha wakati wanakahawa ndani, na hawajui waiuze wapi baada ya serikali kuwataka kukiuzia chama cha ushirika cha Ngara Farmers Cooperative.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa