- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Epukeni mazingira ya kujaribiwa kwa lengo la kuwasadia watahiniwa; kama hamkuwafundisha vizuri waacheni washindwe, kwa sababu itakuwa ndiyo haki yao.” Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele alitoa wito huo kwa washiriki wa kazi maalumu Septemba 05, 2018.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Mntenjele, amesema watoto waliojifunza kwa bidii waachwe wafaulu kwa juhudi zao, huku akiwataka washiriki wa kazi hiyo maalumu kuwa wautulivu, wenye akili pamoja na busara.
“Hakikisheni sifa nzuri ya Wilaya ya Ngara inaendelea kudumishwa, na kuhakikisha hakuna udanganyifu katika mithani kwa kusimamia vema mtihani huu.” Alisema Lt. Col. Michael Mntenjele
Hata hivyo, alisisitiza kwamba anatumaini washiriki hao, wataifanya kazi hiyo nyeti ya kitaifa kwa uadilifu mkubwa, na kwa kuzingatia maelekezo ya kusimamizi mitihani yaliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
Aidha, amesema uteuzi wa washiriki hao, umezingatia mwongozo na taratibu ambao unasisitiza mshiriki lazima awe na sifa zinazokubalika, ambazo ni kuwa mwaminifu na mwadilifu, uzoefu kazini, afya njema, sifa za kitaaluma pamoja na kufanya shughuli hii kwa kuzingatia maadili ya ualimu.
“ Kuteuliwa kwenu kunaonyesha imani kubwa aliyonayo kiongozi wenu katika utendaji wenu wa kazi, uadiili na uamnifu mlionao katika kutimiza wajibu wenu. kwa hiyo ni matumaini yangu kwamba amtaiangusha mamlaka iliyowateua kufanyakazi hii.” Alisema Lt. Col. Michael Mntenjele.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani (W) Ndugu Aidani John Bahama, ametoa wito kwa washiriki hao, kuwa watulivu vituoni na kuacha tabia ya ulevi na vitendo viovu.
“Uzoefu umeonyesha kwamba baadhi yanu tunapowapeleka kwenye vituo vya kazi maalumu, wanadhani ni sehemu ya mapumziko, wanalewa kisha wanasahau kazi iliyowapeleka huko.” alionya Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani (W) Ndugu Bahama.
Ametoa rai kwa washiriki kwamba serikali haitamvumilia mtu anayeacha majukumu, huku akiwataka kuifanya kazi hiyo kwa weledi na uaminifu mkubwa ili hata mwakani waweze kuteuliwa tena.
Akiwa ofisini kwake Afisaelimu Idara ya Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Gideon Mwesiga, amesema mwaka 2018 watainiwa ni 5,095; wasichana ni 2,644 na wavulana ni 2,451.
Amesema kati yao watahiniwa watatu wavulana wawili na msichana mmoja, wana uoni hafifu (Low Vision); ambapo wavulana wanatoka shule ya msingi ya Ruganzo na msichana anatoka katika shule ya msingi ya Muhweza.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa