- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika hafla ya kutambua mchango wa wadau kwenye sekta Elimu ya Elimu iliyofanyika leo tarehe 31 Agost 2023 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ikishirikisha mikoa yote ya Tanzania bara
Mkuu wa Mkoa Kagera Hajati Fatma Mwassa amesema kuwa wadau wa Maendeleo wamechangia shilingi bilioni 6.3 kwa ajili ya kuboresha sekta ya Elimu
Hajati Fatma amewashukuru wadau mbalimbali Mkoani Kagera waliochangia kiasi hicho cha fedha akitaja wachache kuwa ni *Kampuni ya Kabanga Nikel, kiwanda cha sukari Kagera, Shule za Bunazi Green Acres (Missenyi) na Kemibos (Bukoba)*
Hajati Mwassa pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya Elimu nchini vilevile akamhakikishia kwamba michango ya wadau itaboresha miundombinu ya Elimu
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mpango wa Global Partnership for Education (GPE) Tanzania unaotekelezwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa