- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Kagera (TRA) wametakiwa kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wakulipa kodi bila shuruti, badala ya kufunga biashara zao na agizo hilolinatekelezwa kuanzia Januari 2019.
Mkuu wa Mkoa wa KageraBrigedia Jenerali Marco E. Gaguti ametoa agizo hilo Janauri 11, 2019 wakati wakikao cha Baraza la Wafanyabiashara kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa yaBukoba.
Mkuu huyo wa mkoa aliwaitawafanyabiashara hao, ili kusikikiliza kero zao kwa lengo la kuboresha ulipajiwa kodi kwa serikali Mkoani Kagera, pamoja na kufikia malengo ya ukusanyaji wakodi kwa mwaka 2018/2019 kwa asilimia 100%.
Wafanyabiashara walipewanafasi ya kuchangia namna bora ya kuhakikisha kodi inakusanywa kwa asilimia 100%na wafanyabiashara wote wanalipa kodi hiyo katika mazingira rafiki yasiyokuwana bughudha yoyote.
Wafanyabiashara walilalamikia utendajikazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa hawawaelimishi wafanyabiasharaumuhimu wa kutoa kodi ili kuwajengea mazingira mazuri ya kulipa kodi hiyo jamboambalo limepelekea wafanayabisahara wengi kufunga biashara zao.
Baada ya kutoa dukuduku zao, Mkuuwa Mkoa Brig. Jen. Gaguti aliwataka TRA Mkoani Kagera wajenge mazingira mazuri ambayoyatawawezesha wafanyabiashara hao kufanya biashara na kulipa kodi bilakushurutishwa, huku akisistiza kuwepo na takwimu sahihi za wafanyabiashara mkoanihumo.
Alitoa siku kumi na nne kwaMamlaka za Serikali za Mitaa, kuwatumia Viongozi na Watendaji katika ngazi zaKata hadi Vijiji kuwatambua wafanyabiashara wote, ili kuwe na takwimu sahihi yawananchi wanaofanya biashara kwani Mkoa wa Kagera ulipaji kodi ni 0.4% tu.
Aidha, aliitaka TRA kutanua wigo wakukusanya kodi hasa kodi za majengo na ardhi, huku akiwataka wafanyabiasharakuwa wakweli katika kutoa takwimu zao za biashara, ili wasikwepe kodi na walawasionewe.
Mkuu huyo wa Mkoa Brig.Jen. Gaguti aliitangaza tarehe 25 hadi 30 Machi, 2019, kuwa ni wiki ya Mkoa wa Kagerana kuwaomba wananchi katika Sekta zote kushiriki kuutangaza Mkoa wa Kagerakatika wiki hiyo.
Wakati huo huo, Katibu Tawala waMkoa wa Kagera Prof. Faustine Kamuzora, aliwahakikishia Wafanyabiashara uongoziwa mkoa umejipanga kuondoa vikwazo, vinavyorudisha juhudi za wafanyabiashara nyuma,na kwamba serikali ya Awamu ya Tano inataka kila mwananchi anajimudu kiuchumi.
Profesa Kamuzora alisema kuwaatahakikisha anaimarisha Mabaraza ya Wfananyabiashara ya Wilaya na Mkoa ilikuhakikisha Sekta binafsi inashirikiana na Serikali kikamilifu katika kuchumiwa Mkoa na Taifa kwa ujumla
“Jana wakati nimefika hapa mkoaniniwauliza wenzangu kuwa mkoa wetu hivi leo unacheza ngazi gani ya liginikaambiwa unacheza ndondo cup, wakati ule Kagera tulikuwa tunawika katika PremiereLeague, lakini sasa Ndondo? Hapana! hatutakiwi kuwa ndondo tunatakiwakuwa Premiere.” Alisissitiza Prof. Kamuzora
Mara baadaya kikao cha Baraza laBiashara la Mkoa wa Kagera kumalizika Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoapamoja na viongozi wengine, walitemblea baadhi ya Wafanyabiashara kusikiliza changamotowanazokumbana nazo, ili kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mazingira rafiki ya biasharana kulipa kodi kwa utashi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa