- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wafanyakazi wa Watumishi wa Sekta mbalimbali Mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa Juhudi na Maarifa, Ili kuleta matokeo chanya kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassani imeendelea kuwawekea mazingira wezeshi ya Utendaji Kazi.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi Mkoani Kagera, Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Hajat Fatma Abubakari Mwassa, amewakumbusha Wafanyakazi hao Juu ya Mshikamano wakati wa kukabili na kutatua changamoto katika maeneo yao ya Kazi.
Mhe. Mwassa amesema kuwa kila Mfanyakazi ana wajibu wa kufanya kazi kwa bidii umahiri na weledi kwa Kasi inayohitajika ili kupunguza malalamiko kwa Wateja, na kuongeza Ufanisi.
Aidha ameongeza kuwa Serikali inaendeleza jitihada za kulipa haki na stahili za Wafanyakazi kwa Wakati.
Huku akikukumbusha waajiri kuendelea kuchangia mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Wafanyakazi kwa uaminifu na Kuahidi kufuatilia Masuala haya kwenye ngazi husika kwenye Mkoa wake wa Kagera.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Kagera amemtaka Kamishna wa Kazi Mkoani Kagera kufuatilia na kuchukua hatua za haraka kwa waajiri wote Mkoani Kagera ambao wamekuwa na Tabia ya kutolipa mishahara kwa wakati, na wakati mwingine kulimbikiza mishahara ya Wafanyakazi jambo ambalo halikubaliki Kisheria.
Pia kuhusu suala la posho kwa Wastaafu, Mkuu wa Mkoa Kagera mhe Hajat Fatma Mwassa amekiri kuwa Mtumishi anapostaafu anatakiwa kuendelea kuishi kwa heshima, kama Walivyotumikia na Kutoa jasho katika Ujenzi wa Taifa lao, hivyo Serikali imeendelea kuboresha masilahi ya Wafanyakazi kwa kuwapandisha Vyeo, na kwa kuwa posho hutegemea Mshahara wa Mwisho ambao Mtumishi amestaafu akiwa analipwa.
Maadhimisho hayo Kimkoa yamefanyika Manispaa ya Bukoba katika Uwanja wa Kaitaba na kuhudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali ikiwemo Viongozi na Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma, Taasisi Binafsi na Serikali.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa