- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali imetoa fursa kwa wanafunzi waliofaulu kidato cha nnemwaka 2018 na wanaotegemea kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo kwa mwaka2019 kubadilisha Tahsusi(Combination).
Akitoa taarifa kwa vyombo vyaHabari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo Serikali ya Awamu ya Tano inawapa wahitimu hao fursa ya kufanyamabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali walizozichaguakwenye fomu ya “F4-Selform.
Amesema Fursa hii itawawezeshawanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeoya Kidato cha Nne 2018 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania, NECTA.
“Kwa mara ya kwanza Wanafunziwatakuwa na uwezo wa kubadili machaguo au kuchagua kutoka Kidato cha Tanokwenda Chuo au Chuo kwenda Kidato cha Tano kwa kadiri ya mahitaji yake na jinsialivyofaulu mitihani yake” alisema Jafo.
Unajua wanafunzi hujaza Fomu zaF4-Selform kabla ya kufanya mitihani sasa matokeo huweza kuja tofauti na vilealivyojaza lakini mwanafunzi huyo amefaulu hivyo ni wakati sasa kwa kubadilishamachaguo kwa kadiri ya ufaulu wake na anavyopendelea mwenyewe alisisitiza Jafo.
Aidha Waziri aliongeza kuwaOfisi yangu imetoa fursa hii kwa wahitimu kubadili machaguo yao ili kutoamwanya zaidi kwa mwanafunzi kusoma fani au Tahasusi itakayomwandaa kuwa namtaalam fulani katika maisha yake ya baadaye kwa namna ambayo anatamani yeyemwenyewe au kwa kushauriwa na wazazi au walezi wake; Hii ni kutokana na ukwelikwamba baadhi ya wanafunzi hawakujaza kwa uhakika Tahasusi au Kozi zao kutokanana kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao.
Aliongeza kuwa zoezi la awalila kuingiza taarifa zilizo kwenye “Selform” za wanafunzi kwenye kanzidata yaOfisi ya Rais - TAMISEMI, kama zilivyojazwa wakiwa shuleni kabla ya kuhitimulimekamilika na sasa wanafunzi wataweza kufanya mabadiliko kwa njia ya mtandao,(online) na baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hii ndiyoitakayotumika kuwachagua na kuwapangia kidato cha Tano na Kozi za Vyuo.
Waziri Jafo aliwakumbushawahitimu wote kuwa, endapo wanapenda kurekebisha machaguo ya Tahasusi naKozi au kuhama kutoka Chuo kwenda Kidato cha Tano kulingana na ufaulu waokatika masomo wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa Selform unaopatikana katikaanuani ya www.selform.tamisemi.go.tz na maelekezo ya jinsi ya kufanyamabadiliko watayapata kwenye video ya mafunzo inayopatikana kwenye tovutiya TAMISEMI www.tamisemi.go.tz
Pia alifafanua kuwa Ili mhitimuaweze kuingia kwenye mfumo itabidi kutumia namba ya mtihani wa kuhitimu Kidatocha Nne mwaka 2018, jina lake la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama ya ufaulualiyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.
Zoezi hili la kubadilishaTahasusi litafanyika kuanzia tarehe 01/04/2019 hadi tarehe 15/04/2019.
Na - OR-TAMISEMI
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa