- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya fedha, Mipango na Uongozi imeridhika na zoezi la kupasua na kupanua barabara za vitongoji vya Mji wa Ngara, linalofanywa na Tanzania Rural and Urban Roads Agency (TARURA), kwa kushirikiana na Halmashauri kwamba linarahisisha upatikanaji wa huduma za jamii.
Haya ameyasema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Erick Nkilamachumu, wakati akihitimisha ziara ya siku mbili iliyofanyika Novemba 19, 2018 ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo, ,.
“Kwenye suala la barabara changamoto hazikwepeki; kwa sababu tunapopanua barabara tunalazimika kukata migomba, miti na saa nyingine kubomoa baadhi ya nyumba za wananchi, kwa hiyo, lazima lawama ziwepo, lakini lazima tukabiliane nazo.” alisema Ndugu Nkilamachumu.
Amewataka wataalamu kwa kushikiana na Mkurugrnzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, wawasiliane na TARURA, waone jinsi watakavyoweka changarawe na kalavati, ili barabara hizo zipitike wakati wa mvua na kiangazi.
Aidha, amesema wananchi lazima wahamasishwe na kuelimishwa umuhimu wa zoezi hili, kusudi waweze kuhiari kutoa maeneo yao, yatumike katika kupanua na kutengeneza barabara za mji; kwani kufanya hivyo kutarahisisha usambazaji wa huduma za jamii kwa wananchi.
Naye, Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Bi. Georgia Munyonyera, ameishukuru Halmashauri na TARURA, kwa kazi hiyo kubwa na nzuri ya kupasua barabara za mitaa katika maeneo mbalimbali, huku akiomba zoezi hilo liendelee katika vitongoji vingine.
Barabara hizo ni msaada mkubwa, kwa sababu zitarahisisha maisha ya wananchi na kuongeza thamani ya viwanja vyao baada ya kuvipima, huku akitoa ushauri wa jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza, hasa kuhusiana na mashamba ya watu ambako barabara hizo zinapita.
“Nitoe wito kwa wataalamu wa maedeleo ya jamii na ofisi ya mamlaka ya mji mdogo, wawashauri na kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa barabra hizo kwao, ili wawaruhusu na kama kuna tatizo basi tulitatue kabla.” Alisema Bi Munyonyera.
Ziara ya siku mbili ya wajumbe wa kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi, walitembelea miradi Maendeleo; ukamilishaji wa maabara katika shule za sekondari za Murugwanza na Kanazi, Kituo cha Afya cha Mabawe, na vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi ya Rulenge vilivyojengwa kwa msaada wa Jambo Bukoba na Halmsahauri kwa gharama ya shilingi milioni 23.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa