- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakimbizi sita waliofariki kwa ajali wakitokea kambi ya Nduta katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, wakirejea makawao wamezikwa Aprili 03, 2018 Benaco katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Mazishi hayo yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga, akishirikiana na viongozi wa serikali na mashirika ya kuwahudumia wakimbizi, ambapo miili ya wakimbizi hao waliopata ajali ya Basi Machi 29 K9 ilizikwa rasmi.
Wakimbizi waliofariki katika ajali hiyo wamejulikana kuwa ni ndugu Batungwanayo Salvatory (56), Ndugu Bacumi Casmir (52), Ndugu Tuisenge Minani (12), Ndugu Miburo Gervaz (63), Ndugu Nyandwi Veronica (70) pamoja na Ndugu Nyabenda Leonia ((31).
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kigoma amesema vifo vya wakimbizi hao ni pigo kwa nchi zote mbili, kwani walikuwa wakirejea nchini kwao kuendelea kulijenga taifa lao, na maendeleo yao binafsi.
“Kila aliyeguswa na tukio hili naomba alikabidhi kwa Mwenyezi Mungu, kwani safari ya ndugu zetu hawa ilianza bila matatizo yoyote, hadi ilipotokea bahati mbaya hiyo.” Alisema Brigedia Jenerali Maganga.
Aidha, ameyataka mashirika ya kuwahudumia wakimbizi, kwa kushirikiana na serikali, kuhakikisha kwamba kampuni za usafirishaji wanawalipa bima ndugu wa marehemu na waliojeruhiwa katika ajali hiyo.
Amesema zoezi la kuwarejesha wakimbizi makwao kwa amani na utulivu litaendelea pamoja na ajali hiyo kutokea ili wakimbizi wakaungane na wenzao kuijenga nchi yao ya Burundi.
Idadi ya vifo vya wakimbizi waliopa ajali Machi 29, 2018, kwenye mteremko wa K9 katika kijiji cha Kasharaza wilayani Ngara, waliongezeka na kufikia wanane baada ya wawili kufariki katika Hospitali ya Murugwanza.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa