- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mh. Pierre Nkurunziza amewahakikishia warundi wote kuwa kwa sasa nchi ya Burundi ina amani, kwa hiyo wale wote waliokimbia warudi nyumbani kuijenga nchi yao. Ameyaeleza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Posta ya zamani wilayani Ngara. Mkutano ulihudhuriwa pia na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli, mawaziri kutoka nchi hizi mbili wa wizara za Ulinzi, Ujenzi, Mambo ya ndani, Fedha na Mipango na naibu waziri wa Mambo ya nje kwa upande wa Tanzania.
Rais Nkurunziza ameeleza kuwa takribani warundi laki moja na nusu walirudi nyumbani kwao Burundi kwa hiari bila msaada wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), hali inayoonesha kuwa kwa sasa kuna amani katika nchi hiyo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa