- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Wakuu wa shule za sekondari za kidato cha IV wasibweteke na matokeo waliyoyapata mwaka huu, badala yake waongeze juhudi, ili lengo la Halmashauri ya Wilaya ya Ngara la kufuta daraja la III na IV litimie.” Alisema Kaimu Afisa Elimu Sekondari Ndugu Martin James.
Ndugu James akiwa ofisini kwake Julai 2018, amewapongeza wakuu wa shule kwa kazi nzuri waliyoifanya, kwani shule 04 kati ya 05 za kidato cha IV katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, zimejitokeza kati ya 10 bora kimkoa.
Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita katika mwaka wa masomo 2017/2018, wilayani Ngara wamefaulu kwa kupata daraja I hadi la III, ambapo wanafunzi 5 pekee ndiyo walipata daraja la IV na hakuna ziro.
Amefafanua kwamba kimkoa shule ya sekondari ya Rulenge imekuwa ya 03 na imekuwa ya 31 kitaifa kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo; huku ikiwa na wanafunzi 13 waliopata daraja la I, daraja la pili 25 na la tatu 03 hakuna daraja la 04 na ziro.
Shule nyingine ni Lukole ambayo imekuwa ya 05 kimkoa na kitaifa ikawa ya 89 kwa kuwa na wanafunzi 42 waliopata daraja la kwanza, daraja la pili 195 na la tatu wanafunzi 59; shule ya sekondari Muyenzi imekuwa ya 06 kimkoa na kitaifa ikawa ya 99 kwa kupata daraja la kwanza 03, la pili 50 na la tatu 11 hakuna daraja la IV na ziro.
Shule ya sekondari Kabanga imeshika nafasi ya 10 kimkoa na kitaifa imekuwa ya 195 kwa kupata daraja la kwanza 20, la pili 73, la tatu 52, daraja la IV 04 hakuna ziro; huku shule ya sekondari ya Murusagamba imekuwa ya 13 kimkoa na kitaifa imeshika nafasi ya 248 kwa kupata daraja la kwanza 03, la pili 26, la tatu 18 na daraja la IV mmoja tu hakuna ziro.
Aidha, Kaimu Afisaelimu huyo amesema kwamba kufuatia maandalizi waliyofanya na wakuu wa shule za sekondari na idara ya elimu sekondari, anatumaini matokeo ya kidato cha IV mwaka 2018 watafanya vizuri kama ndugu zao wa kidato cha VI.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa