- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakuu wa Idara na Vitengo Vya Halmashauri wakiongozwa na kaimu Mkurugenzi Ndg. Emmanuely Kulwa, pamoja na Diwani Mhe Raurent John wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Murubanga Sekondari iljyopo kata ya Nyamagoma Wilayani Ngara.
Ujenzji wa shule hiyo Umekamilika na umeghatimu tsh 584,280,028 (SEQUIP)
Viongozi hao wametembelea kuona maabara 3 za physics, Chemistry na Biology pia vyumba 8 vya Madarasa, Jengo la Utawala , Maktaba 1, chumba Cha kompyuta 1, matundu ya vyoo 20, viti na meza za wanafunzi.
Mhe Diwani ameishukuru Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanii Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta Fedha za kujenga shule Mpya na Mzuri yenye mvuto.Aidha aliendelea Kwa kusema shule hii itaondoa adha kubwa waliyokuwa wakiipata wanafunzi kutoka kata ya Nyamagoma kwenda shule ya Sekondari Murusagamba umbali wa takribani kilometa 15.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakiangalia maabara shule ya Sekondari Mpya Murubanga kata ya Nyamagoma.
Viti na meza vikiwa tayari kwa ajili ya wanafunzi kidato Cha kwanza 2024.
Viongozi kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Emmanuely Kulwa, Ndg Stivin Mhina Afisa ugavi, mwl Enock Ntakisigaye Afisa elimu Sekondari na Mhe Diwani Raurent John wakiangalia viti na meza vikiwa Darasani.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg Emmanuely Kulwa kulia , na katikati Ndg Constantine Msemwa Afisa Mipango Halmashauri wakiwa shule Mpya ya Sekondari Murubanga.
Vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Mpya Murubanga kata ya Nyamagoma.
Shule ya Sekondari Mpya ya Murubanga kata ya Nyamagoma.
Vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Murubanga.
Viongozi wakitembelea Maabara.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa