- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakuu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wameagizwa kusimamia kanuni na taratibu za ufundishaji, ili kuongeza ufaulu kwa kufuta daraja la nne na ziro katika mitihani ya taifa.
Hayo yameagizwa na Kaimu Afisaelimu Idara ya Sekondari Ndugu Marton James Machi 15, 2018, wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Ngara, kikiwajumuisha walimu wakuu wa shule zote za sekondari wilayani humo.
Kikao hicho kililenga kutoa maelekezo na kujadili mbinu mbalimbali za kuongeza ufaulu katika shule za sekondari, ikiwa ni pamoja na kuogeza ufaulu kwa daraja la kwanza na la pili pekee.
“Wakuu wa shule mnatakiwa kusimamia kazi zenu ipasavyo, kwani baada ya kutembelea shule zenu tumegundua kuwa walimu wengi hawana maazimio ya kazi, maadalio ya masomo, na hamsimamii mazoezi ya kila siku.” Amesema Ndugu James.
Amewataka wakuu wa shule kuwahimiza walimu kuandaa maswali yanayokidhi ubora, na kuwashauri kuyapitia katika kamati za mitihani, ili yawe na ubora unaotakiwa.
Amewasistiza kusimamia kikamilifu shughuli za kitaalauma na kiutawala, huku wakilenga kubaini mapungufu na kuyaondoa kabisa.
Aidha, katika kikao hicho, wakuu hao wa shule wametakiwa kujenga mahusiano mazuri na walimu, kwa madai kuwa wakiwatenga walimu hao hawatafikia malengo yao.
Wakati huo huo, wakuu wa shule wamewahakikishia maafisaelimu idara ya sekondari wilaya, kwamba vijana wanasoma kwa bidii, na kwamba mwaka huu wilaya itakuwa ya kwanza kimkoa.
Vile vile wameushukuru uongozi wa elimu wilaya kwa kuwaarika katika kikao cha kazi, kwani kwa pamoja wanapata nafasi ya kuyajadili mapungufu na kuyatafutia ufumbuzi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa