- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wazazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wametakiwa kuwaleta watoto wa kike wenye umri wa miaka 14, ili waweze kupata chanjo ya kuwakinga na maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi, polio pamoja na suluha.
Akionge wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo katika hospitali ya Rulenge Aprili 23, 2018, Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Aidan John Bahama, amesema kwamba chanjo hiyo ni muhimu na kuwataka wazazi kutowazaui watoto hao kupata chanjo hiyo.
“Niwaombe wazazi wa watoto ambao hawako shuleni, lakini wamefikia umri wa kupata chanjo hiyo wawalete wachanjwe, kwa sababu chanjo hii ni muhiumu ingawa umuhimu wake, hauonekani kwa sasa.” Alisema Ndugu Bahama.
Amewahakikishia wazazi wote kwamba chanjo hiyo haina madhara yoyote, kwani imezinduliwa na serikali, na kuongeza kwamba watu wanaweza kudhani chanjo hiyo si salama.
Aidha, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngara Ndugu Vedastus Tibaijuka, ameishukuru serikali kwa kwa juhudi inazozifanya katika kuimarisha afya ya wananchi wake.
Amesema vijana wengi wana afya nzuri; hawana mangonjwa kama ilivyokuwa zamani, kwani wengi wao wangekuwa walemavu wa viungo, lakini sasa hivi afya yao imeimarika.
“Sasa niwaombe wale wazazi wanaowaficha watoto wasipate chanjo waache tabia hiyo, na mara moja wawalete watoto wa kike wenye umri stahiki wapate chanjo hiyo.” Alisema ndugu Tibaijuka.
Wilaya ya Ngara imelenga kuchanja watoto wa kike wenye umri wa miaka 14, wapatao 7575 kutoka katika shule 145 za sekondari na za msingi.
Chanjo hiyo imezinduliwa Aprili 23, 2018 na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele na kuhudhuliwa na Katibu Tawala, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani, wafanyakazi wa idara za afya, pamoja na wanafunzi wa sekondari za Lake na Rulenge.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa