- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Walimu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wanaohamia shule za msingi wamekumbushwa kwamba uhamisho huo si wa adhabu, bali ni kwa ajili ya kupunguza tatizo la walimu katika shule hizo.
Kaimu Afisaelimu Idara ya Sekondari Ndugu Marton James ameyasema hayo, wakati akiongea na walimu wakuu wa shule za sekondari, kwenye kikao cha kazi kilichofanyika Machi 15, 2018, katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Ngara.
“Niwaombe Wakuu wa shule za sekondari muwajenge walimu hao kisaikolojia, kwamba uhamisho huo unalenga kuongeza nguvu katika shule zetu za msingi wala si wa adhabu.” Alisema Ndugu Marton.
Amesema kuwa walimu wa masomo ya sanaa katika shule za sekondari ni wengi, wakati katika shule za msingi kuna upungufu, hali iliyoplekea baadhi ya walimu hao kuhamishiwa shule za msingi.
Wakati huo huo, wazazi katika Halmashashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuhakikisha wanafunzi wa sekondari wanapata chakula cha mchana shuleni, ili kiwasaidie kufuatilia masomo yao kwa umakini.
“Chakula kitolewe kwa wanafunzi bila walimu kuchangisha fedha za chakula, bali wazazi wahakikishe watoto wanapata mlo wa mchana shuleni.” Amesema ndugu marton.
Aemsema ukosefu wa chakula cha mchana ni moja ya sababu zinazopelekea watoto wengi kuwa watoro, kwani inakuwa vigumu kwao kufuatilia masomo, huku wakiwa na njaa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa