- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii wameshauriwa kuwa kielelezo katika kuelimisha jamii umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti halali yenye thamani halisi ya huduma aliyeipata.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.
"Mitandao ya Kijamii imekuwa nyenzo kubwa ya kuifikia jamii kwa haraka na kwa ukubwa hivyo niwaombe mtumie fursa hiyo kuielimisha jamii umuhimu wa kudai risiti yenye thamani halali ya huduma uliyeipata,"amesema Mwaipaja
Pia amewataka wanamitandao hao kuisaidia serikali kuwaelimisha jamii kuhusu agenda ya maendeleo ya taifa na miradi inyotekelezwa na serikali kwa ajili ya maslahi ya watanzania ikiwemo miradi ya Kimkakati.
Aidha amewapongeza kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha katika kuhabarisha Umma juu ya mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara hiyo.
"Wizara inawatambua nyie ni wadau muhimu sana katika kutoa taarifa zetu na mmekuwa mkifanya hivyo siku zote na jamii imekuwa ikipata taarifa kupitia mitando yenu bila kuda chochote kwa hilo niwapongeze sana"ameeleza
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kongamano hilo Ndg Mathias Canal ameipongeza wizara ya fedha kwa kuandaa kongamano hilo la siku mbili litakalowakutanisha waandishi wa habari za mitandao na kusema kuwa hiyo itakuwa fursa ya kurahisisha utendaji kazi wao kwa umma.
Canal ameitaka wizara ya fedha kuhakikisha kuwa inatoa ufafanuzi kwa umma kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na umuhimu wa mikopo ili kuondoa sintofahamu kwa jamii kuhusu mikopo ya serikali.
''Umuhimu wa kupitishwa kwa sheria ya marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2023 ambapo amesema Masharti yaliyokuwemo yalisababisha kuwepo kwa ushiriki hafifu wa Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa utaratibu wa ubia.''amesema Bw.Canal
Aidha amewataka waandishi hao kutoa taarifa kwa kina katika jamii kuhusu umuhimu wa kulipa kodi, pamoja na kudai risiti kwa kila bidhaa wanazonunua.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa