- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi wa kidato cha sita na wasimamizi wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuwa waadilifu, ili mitihani ya kidato cha sita iweze kufanyika kwa amani na ututlivu.
Kaimu Afisaelimu Idara ya sekondari Ndugu Marton James, ameseyama haya Mei 07, 2018 ofisini kwake, kwamba wanafunzi 599 wa kidato cha sita kutoka katika shule 05 za selikari na binafsi wameanza mitihani yao Mei 07.
Ndugu James amesema kwamba katika Halmashauri ya Wialaya ya Ngara wanafunzi hao wanatarajia kumaliza zoezi hilo maalum Mei 21, 2018, ambapo wenzao hapa nchini watakamilisha zoezi hilo Mei 24, 2018
Ili zoezi hilo lifanikiwe hakuna budi watendaji wote, kuanzia wanafunzi wanaofanya mitihani hiyo, wasimamizi na hata madereva wanaosambaza mithani hiyo, imewapasa kuwa waadilifu na makini wakati wote wa zoezi hili.
“Wanafunzi hao wanatoka katika vituo vitano ambavyo ni shule ya sekondari Kabanga, Rulenge, Lukole, Muyenzi na Murusagamba; kati ya shule hizo ya binafsi ni Rulenge inayomilikiwa na Jimbo Katoliki la Rulenge.” Alisema Ndugu James.
Aidha, amesema wanafunzi wa kujitengemea 45 wanaofanya mitihani yao katika vituo vya Rulenge, Kabanga na Muyenzi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa