- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Murugwanza katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara wameishukuru serikali kwa kuwajengea madarasa manne, mabweni mawili pamoja na kukarabati maabara za biolojia, kemia na fizikia.
Shukurani hizo walizitoa kwa Mkurugenzi Mtandaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, alipotembelea shule hiyo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya afya na elimu, ili kujiridhisha na maendeleo ya miradi hiyo Mei 24, 2018.
Wanafunzi hao wamesema mabweni yamewasaidia wanafunzi waliokuwa wakiishi mbali na shule, kuwahi vipindi darasani, kuwa na utulivu wa mawazo, kujisomea kwa bidi pamoja na kupata nafasi ya kujadili masomo na wanafunzi wenzao.
“Sisi wanafunzi wa kike tulikuwa tunapata shida sana, mbali na kutembea umbali mrefu kuja shuleni, njiani tulikuwa tunakutana na vishawishi vingi, lakini sasa tunatarajia kufanya vizuri katika mitihani yetu baada yak upata nafasi ya kulala shuleni.” Mwanafunzi mmoja wa kike alimwambia Mkurugenzi Mtendaji.
Aidha, walisema kuwa bado tatizo la upungufu wa mabweni lipo, kwani wanafunzi wengi bado wanatembea umbali mrefu kuja shuleni, kwa sababu hiyo wengi uchelewa kuhudhuria vipindi vingi vya kwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, amesema mradi wa ujenzi wa mabweni mawili (02) yenye uwezo wa wanafunzi 80 kila moja, madarasa manne (04), na ukarabati wa maabara vimegharimu shilingi 292,000,000/=.
Amewaambia wanafunzi hao kuwa serikali inalengo la kujenga mabweni ya wanafunzi kwa kila shule, lakini itafanya hivyo kwa awamu, hivyo aliwataka wanafunzi hao kuwa wavumilivu, wakati serikali inajipanga kukamilisha mabweni katika shule zao.
Mkurugenzi Mtendaji alikuwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mei 22-25, 2018 na kulidhishwa na maendeleo ya miradi hiyo, kwani yote ipo katika hatua za usafi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa