- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 8 Agosti 2019 timu ya wahamasishaji wa kampeni ya Nyumba ni Choo ilibisha hodi katika Kata ya Muganza kijiji cha Ruhuba kwa lengo la kuelimisha wananchi juu ya matumizi bora ya choo na umuhimu wa kuwa na choo bora.
Kijiji hiki ambacho katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019, vyoo bora ilikuwa ni 84 ambavyo ni sawa na aslimia 6.1. Vyoo vya asili ni 1285 sawa na asilimia 93.9. Kaya zinazonawa mikono kwa maji tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni ni 108 sawa na asilimia 7.9 tu.
Akitoa elimu ya choo bora, Ndugu Salum Kimbau ambae ni Afisa Afya Wilaya aliwataka wanakijiji wae na desture ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni. "Choo bora hakina gharama wala hakihitaji fedha nyingi ili kukikamilisha,nawaomba Ndugu zangu tuwe na vyoo bora maana ni faida kwa afya zetu na jamii yetu yote",Aliongezea Afisa Afya Wilaya.
Baada ya elimu iliyotolewa na wahamasishaji, wanakijiji kwa pamoja wakiongozwa na Mtendaji wa Kijiji, walikula kiapo na kusema ifikapo tarehe 9 Septemba 2019 watakuwa wamefikia Asilimia 100 ya vyoo bora.
Kabla ya kufunga kampeni hizo,Mwenyekiti wa kijiji cha Mukubu aliwaomba wanakijiji kuzingatia elimu walioipata kutoka kwa wahamasishaji na alisisitiza kupita kila kaya kukagua kama kiapo walichoapa mbele ya wataalam kinafanyiwa kazi.
..........................................USICHUKULIE POA,NYUMBA NI CHOO............................................................
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa