- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Michezo ya watumishi Mamlaka ya serikali za mitaa ( SHIMISEMITA) Kitaifa iliyofanyika Mkoani Morogoro kuanzia tarehe 18/10_31/10/2022.kwa kushirikisha Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji 57 kati ya 187. Wilaya ya Ngara alipeleka wanamichezo 18 na viongozi 3 . Ngara ilishiriki katika michezo ya Netiboli, Riadha, Bao,na karata. Wilaya ilifanya vizuri katika michezo ya riadha na karata wanaume ambapo wilaya ilipata nafasi ya pili kitaifa katika mchezo wa Jadi / Asili karata.
Kwa upande wa Riadha mbio mita 100 Bwana Julius mkumbo kushika nafasi ya tatu kitaifa , na Bw Bahati Michael kushika nafasi ya 4 kitaifa mita 100 pia Bi. sarafina alishika nafasi ya 3 kitaifa mbio mita 100.Alipongezwa Bw solomon Kimilike mkurugenzi mtendaji kwa kuwa wilaya pekee katika mkoa wa kagera iliyoshiriki michezo ya watumishi.
Wanamichezo hao wamekabidhi cheti na kikombe kwa Bw solomon kimilike, aidha baada ya kupokea aliwashukuru sana wanamichezo kwa kuheshimisha wilaya yetu kwa kurudi na kikombe na kuahidi mwakani maandalizi yaanze mapema ili kufanya vizuri .
Mratibu wa michezo Bw Said Salum alieleza kuwa mwakani ili kujiandaa ni kuanzisha Ded cup kwa kushindanisha idara kwa idara ili kupata wachezaji mahili wa michezo mbalimbali. Wanamichezo walimpongeza sana Mlezi wa timu ya Halmashauri sport club Bw Solomon kimilike Mkurugenzi mtendaji kwa kutoa usafiri ,posho kwa wanamichezo ,pia kuwashukuru Bi Sabra Mwankenja Afisa utumishi kwa hamasa kwa wanamichezo, kabla ya kuondoka kuelekea Morogoro.
Wanamichezo pia waliwapongeza Bw. Msemwa Constantine Afisa mipango wilaya na Bw. Abbas Yusuf mweka hazina wilaya kwa kufika kuhamashisha na kutoa maji tsh 100,000= Mwisho walimshukuru Mhe Oliva Semuguruka Mbunge viti maalum Mkoa wa kagera kwa kutoa Maji kwa wanamichezo Tsh 200,000=.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa