- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wamefurahishwa na kuridhishwa na matokeo ya miradi ya TASAT, inayoendelea kutekelezwa wilayani humo baada ya kunufaika na malengo ya miradi hiyo.
Hayo yamesemwa na walengwa wa miradi hiyo Mei 07, 2018, katika vijiji mbalimbali wilayani Ngara, wakati wafanayakazi wa TASAF ngazi ya wilaya, walipokuwa wakikagua mradi wa kupanda miti katika vijiji vilivyo chini ya miraid ya TASAF.
Wamesema kwamba TASAF ni mkombozi kwani kaya nyingi ambazo zilikuwa hazina matumaini ya maisha, sasa zimeinuka na kwamba kaya hizo zina uhakika wa chakula, sare za shule kwa watoto wao, na wameezeka nyumba zao kwa bati kinyume na ilivyokuwa kabla ya mradi wa TASF.
Aidha, mradi wa kuoanda miti kwa lengo la kutunza mazingira, unaendelea vizuri kwani miti mingi inaendelea vizuri, ingawa kuna changamoto walizozitaja kuwa miti mingi inaaribiwa na mchwa, mifugo na katika baadhi ya vijiji miti iliyopandwa inashambuliwa na sungura.
Wamesema kwamba wamjaribu kutumia dawa kuua, bila mafanikio kwani wadudu wadudu hao wameendelea kufanya uaribifu, hivyo wameiomba Halmashauri iwabadilishie dawa ili waweze kuokoa miti hiyo.
Akiffanua mtunza shamba wa kijiji Kasange katika kata ya Kirusha Ndugu Juma Abdul, amesema katika awamu ya kwanza wamepanda jumla ya miti 4680 na awamu ya pili wamepanda miti 640, lakini karibu miti ipatayo 1000 imeliaribiwa na mchwa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa