- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi Wilayani Ngara, wametakiwa kuwa wavumilivu wakati baadhi ya barabara za mjini Ngara zimefungwa, kwa ajili ya kuzitengeneza kwa kiwango cha lami.
Mhandisi wa Tanzania Rural Roads Agency (TARURA) Ndugu Christopher Masunzu, amesema hayo ofisini kwake Machi 15, 2018, kwamba wamefunga baadhi ya barabara, ili kupisha ujenzi unaoendelea.
“Tunasikitika kufunga barabara tatu ya kutoka Benki ya National Microfinance Bank (NMB) hadi Halmashauri, kutoka Halmashauri kwenda Magereza, na Mandela Road.” Alisema Mhandisi Masunzu.
Amesema barabara hizo zenye urefu wa Kilomita moja zitagharimu shilingi milioni mia tatu na nne mia mbili sabini na tisa elfu na mia mbili ishirini (304,279,220/=).
Aidha, amesema mkandarasi M/S Jensen Associates (T) wa Dar-Es=Salaam, amesaini mkataba Februari 7, 2018 anatarajiwa kukabidhi kazi hiyo ifikapo Mei 7, 2018.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa