- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, amewaagiza watendaji wa kata na vijiji, kuwataarifu wananchi wenye mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekari hamsini (50), waandike barua ya kuomba ridhaa ya kuyamiliki mashamba hayo.
Akiongea ofisini kwake Machi 21, 2018 kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Afisa Ardhi wa Halmashauri hiyo Bi. Beatrice Mnuo amesema kwamba kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya kijiji namba 5 ya mwaka 1999, kijiji kina uwezo wa kumilikisha na kutoa hati miliki ya ardhi.
“Kijiji kina uwezo wa kugawa na kusimamia ardhi, ambayo iko kwenye mipaka yake, na kimepewa mamlaka ya kutoa hati miliki za kimila kwa wananchi wenye mashamba yasiyozidi ekari 50.” Alisema Bi. Mnuo.
Aidha, kwa mujibu wa maagizo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, wakati wa ziara yake wilayani Ngara, umilikishaji wa mashamba hayo, unatakiwa uwe umekamilika mwishoni mwa mwezi Mei 2018.
Amesema kuwa Halmashauri haitayakubali maamuzi yatakayotolewa bila kumhusisha Mkuu wa Wilaya, na kuongeza kuwa watu wasio raia wa Tanzania, hawataruhusiwa kumiliki ardhi kwa utaratibu huu.
Amesema wananchi wanaomiliki mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 50, wanatakiwa kuhawilisha ardhi, ili wapewe hati miliki ya Kamishina, na ameongeza kuwa lazima waombe ridhaa ya wanakijiji.
Wananchi hao wametakiwa kuwasilisha maombi yao ndani ya mwezi Machi 2018, ili mwezi Aprili 2018 vikao vya serikali za vijiji na mikutano mikuu ya vijiji, viweze kufanya maamuzi na kuyawasilisha kwenye mkutano mkuu, utakaowahusisha Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa