- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Walimu wa shule za sekondari katika Halamsahuri ya Wilaya ya Ngara kwa kupitia ofisi ya mkuu wa shule wametakiwa kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi watakao fanya mitihani ya taifa mwaka huu, ili yawasaidie kujiandaa vyema kwa ajili ya mitihani ya kitaifa.
Kaimu Afisaelimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Marton James ameyasema hayo ofisini kwake Mei 28, 2018, wakati akifafanua ni kwa nini ofisi yake imeamua kuandaa mitihani ya Mock katika wilaya ya Ngara.
Ndugu James amesema wameamua kufanaya mitihani ya Mock kiwilaya kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha nne ili kuwaandaa wanafunzi hao kwa ajili kufanya mitihani ya Mock kimkoa itakayofanyika Julai mwaka huu.
“Mitihani ya mock kiwilaya inatusaidia kujua mapungufu ya wanafunzi na walimu wetu ili tuweze kuyafanyiakazi na kutoa maelekezo yatayosaidia shule zetu za sekondari kufanyavizuri zaidi kwenye mitihani yao ya kimkoa na ile ya kitaifa.” Alisema ndugu James.
Amesema wanataka kubadili matokeo ya kidato cha nne kuonoda kabisa daraja la IV na ziro katika shule zote za sekondari wilayani Ngara mwaka 2018 na wanafunzi wote wapate daraja la I, II na la III pekee.
Amesema katika matokeo ya Kidato cha sita 2012 matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: - wanafunzi wawili walipata daraja la kwanza, daraja la pili walikuwa wanafunzi 34, waliopata daraja la tatu walikuwa wanafunzi 95 na daraja la IV walikuwa wanafunzi 14.
Kaimu Afisaelimu amefafafnua kwamba katika matokeo ya kidato cha nne 2012,wanafunzi 2 walipata daraja la kwanza,wanafuzi 20 walipata daraja la pili,wanafunzi 94 walipata daraja la tatu, wanafunzi 792 walipata daraja la 4 na wanafunzi 1015 walipata ziro/sifuri.
Aidha, akasema kwamba idadi ya ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha pili 2012 uliongezeka hadi 57.2% toka 31.3%, mwaka 2011.
Hata hivyo, amesema kwamba upungufu wa walimu ni tatizo kwani baadhi ya walimu wanaopagiwa vijijini uripoti na kuondoka, kwa madai kwamba mazingira magumu ya utendaji kazi kama vile; ukosefu wa nyumba za watumishi na huduma za kijamii (Maji, umeme hospitali na maduka).
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ina jumla ya shule 29, ambapo shule 23 zinamikiwa na serikali, shule 6 ni za binafsi. Kanisa Katoliki linamiliki shule 2, Kanisa la Anglikana linamiliki shule 01 na watu binafsi wanamiliki shule 03.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa