- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, imewataka watendaji wa kata na wa vijiji wahakiki kwa umakini, kuwepo kwa vikundi vya kijamii, kiuchumi na sanaa vya akina mama, vijana na walemavu kabla ya kuwapitishia usajiri wao.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Josephine Lusatira, amesema hayo Novemba 21, 2018, ofisini kwake; kwa kudai kwamba uamuzi huo umekuja, ili wajiridhishe wakati wanafanya mchakato wa kusajiri na kuvikopesha wa vikundi hivyo.
“Tunawaomba WEO na VEO watusaidie kujua uhalisia wa kuwepo kwa vikundi hivyo, ili tuweze kuvipatia mikopo, kwani serikali inawasadia watu wanaofanya shughuli zao katika vikundi na siyo mtu mmoja mmoja.” Alisema Bi. Lusatira.
kutokana na sheria ya fedha namba 04 ya mwaka 2014, iliyoanza kutumika rasmi Julai 01, 2018, vikundi vyote vitakavyopewa mkopo, vitarejesha mkopo huo bila riba katika muda wa mwaka mmoja.
Amewataka wanavikundi hao kuwa makini, waamini na waadilifu, kwani fedha za mikopo si zawadi inabidi zirejeshwe, ili vikundi vingine viweze kupata mikopo kwa lengo la kuviinua kiuchumi.
“Fedha za mikopo zinatakiwa kuzunguka katika vikundi mbalimbali, alichokitaja kuwa ‘revolving Gunds’; hivyo, ukikopeshwa rejesha kwa muda, ili fedha hiyo ikopeshwe kwa wanavikundi wengine.” Alisema Bi. Lusatira.
Hata hivyo, amesema zoezi hili limeleta changamoto, ambazo baadhi yake amezitaja kuwa vikundi vinavyopitishwa kusajiliwa na kupewa mikopo havina sifa zinazostahili, ambazo amesema kuwa hawafanyikazi kama vikundi bali kila mmoja na shughuli yake.
Umri wa wa wanavikundi nao, ni changamoto, hasa vijana wenginwao wana umri zaidi ya miaka 35 ambapo umri unaotakiwa ni kuanzia miaka 15 – 35, kwani wenye umri zaidi ya huo wanakuwa katika kundi la wazee.
Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, inatarajia kutoa mikopo kwa vikundi vya akina mama, vijana na walemavu hivi karibuni mara taratibu za kutoa mikopo hiyo kwa vikundi hivyo zitakapokamilika.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa