- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Watumishi wa Umma Mkoani Kagera wametakiwa kuyatumia Vyema Mabaraza ya Wafanyakazi ili kuweza kuimarisha mahusiano kazini ikiwa ni chachu ya kutekeleza vyema majukumu na wajibu wao wa kila siku.
Akizindua Baraza jipya la Wafanyakazi Mkoani Kagera, mapema Machi 04 mwaka huu katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa KAGERA, Mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Abubakari Mwassa amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi ni nyenzo muhimu kati ya kuimarisha Uhusiano baina yao na Waajiri Pamoja na Watumishi wengine wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni sambamba na kuimarisha mahusiano ya Taasisi husika.
Aidha Mhe. Mwassa Ameongeza kuwa Mabaraza haya yamekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza maelewano mazuri mahala pa kazi, ambapo migogoro mingi imekuwa ikishughulikiwa kupitia mabaraza haya hivyo kusaidia kuepuka migomo isiyokuwa ya lazima.
Pia Mhe. Mkuu wa MKoa Kagera amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akishughulikia masilahi ya Watumishi ikiwa ni sambamba na Kuwapandisha Watumishi Vyeo na kuinua masilahi ya Wafanyakazi
kwa kurekebisha na kulipa mishahara kwa wakati, pamoja na malipo ya malimbikizo ya madeni ya mishahara.
Katika Hotuba yake Mhe Mwassa amesisitiza Zaidi upendo baina ya Watumishi wenyewe na kuwataka pale penye changamoto wakae chini na kujadili na kuzitafutia ufumbuzi
Awali kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mwnyekiti wa baraza hilo la wafanyakazi Katibu Tawala wa Mkoa Kagera Dkt. Toba Nguvilla
Amekumbusha majukumu ya Baraza hili kuwa ni kuwashirikisha wafanyakazi wa serikali katika utekelezaji wa shughuli za serikali na uongozi, uishauri Serikali juu ya ufanisi wa kazi na hatua zinazofaa kuchukuliwa.
Mhe Hajatt Fatma A Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akiwa kwenye Kikao.
Katibu Tawala mkoa wa kagera Dkt Toba Nguvila akiongea kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Mhe Hajatt Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa kagera.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa