- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Meneja wa TANESCO wilayani Ngara na Mkadarasi wa Wakala wa Umeme nchini, anayesambaza umeme wa bei nafuu (REA) awamu ya tatu kwa wananchi wilayani humo, wameagizwa kuhakikisha kwamba kila mtu aliyelipia umeme anapewa huduma hiyo.
Waziri wa Nishati Mh. Dr. Medard Kalemani ametoa maagizo hayo June 09, 2018, katika kata ya Kasulo kijijini cha Kasharazi Kitongoji cha Gwingwe, alikokwenda kuzindua umeme wa bei nafuu kwa wananchi (REA).
“Hakuna atakayerukwa tunakwenda kijiji kwa kijiji kitongoji kwa kitongoji na nyumba kwa nyumba, kwa hiyo kufikia mwezi Juni mwaka 2019, vijiji vyote 36 wilayani Ngara vilivyopo chini ya wakala wa umeme nchini (REA) lazima viwe vimwekewa umeme.” Alisema Waziri Kalemani.
Dr. Kalemani amesema mardi wa REA awamu ya tatu utasambaza umeme katika vijiji 36, ambapo mwanzoni wilaya ya Ngara ilikuwa imetengewa vijij 21, na katika awamu hii vimeongezeka vijiji 15 zaidi.
Aidha, amsema kwamba serikali inawajibika kwa wananchi inapeleka umeme kwa kila kitongoji, lakini kazi hiyo haiwezi kukamilika kwa siku moja, niwaombe wakandarasi, pamoja na meneja TANESCO wasimamie hiyo kazi kwa nguvu.
Amesema kwamba nyumba nane zilizowashwa umeme siku hiyo, ni chache sana, kwani lengo la serikali ni kila kitongji wilayani Ngara kipate umeme na kwamba haijalishi ni nyumba ya aina gani bali kila atakayelipia umeme awekewe umeme huo.
“Tunataka kukuza uchumi wa taifa, na wa mwananchi mmoja mmoja, lakini hatuwezi kufanya hivyo kama wananchi hawana umeme, pia tunataka wananchi wauze unga badala ya mahindi. Alisema Waziri Kalemani
Ndugu Kalemani ameambatana na wataalamu wa shirika la umeme nchini (TANESCO), ambao ni Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO makao makuu Dar-er-salaam, na meneja wa TANESCO Kanda ya ziwa.
Wengine ni Meneja wa TANESCO mkoa wa Geita, Meneja wa TANESCO mkoa wa Kagera, Meneja wa TANESCO wilaya ya Biharmulo na Meneja wa TANESCO wilaya ya Ngara pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa