- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
FRIIUP COMPANY (T) LTD ya Nchini Korea Kusini yaahidi kutoa ajira za kudumu kwa watanzania wapatao 2500, wakati itakapoanza shughuli zake rasmi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara katika kipindi cha miezi tatu ijayo.
Mkurugenzi Mtandaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan J. Bahama, amesema hayo baada ya uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na wa kampuni ya FRIIUP COMPANY (T) LTD ya Nchini Korea Kusini, kusaini mkataba wa kuwekeza katika kilimo.
“Leo Septemba 03, 2013 tumesaini mkataba wa uwekezaji niseme kwamba, ni uwekezaji mkubwa katika mambo mbalimbali; katika kahawa, mpunga, amakademia na uwekezekaji kwenye avocado.” Alisema Ndugu Bahama.
Ndugu Bahama amesema uwekezekaji huo utachukua ekari takribani 12, 000, na utagharimu dola za kimarekani zipatazo $5,000,000, ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 10,000,000,000 za kitanzania.
Kadiri ya Mkurugenzi huyo Mtendaji mradi huo utakuwa na faida kwa Halmashauri, Wananchi wa Wilaya ya Ngara pamoja na kwa watanzania; na kwamba wameahidi kuiwezesha Halmashauri ya Wialaya ya Ngara katika miundombinu ya barabara, hospitali, pamoja na elimu.
“Tayari konteina moja la kompyuta linakuja kwa ajili ya kuzigawa mashuleni; kompyuta hizo zinatupa uhakika wa watoto wetu kujifunza somo la TEHAMA; kwa hiyo unaweza kuona jinsi uwekezaji huo utavyokuwa na faida kubwa kwetu sisi kama halmashauri.” Alisema Ndugu Bahama.
Aidha, amesema kwamba watu wanaozunguka mradi huo, watawezeshwa katika teknolojia ya kuzalisha kahawa, avocado, makademia na mpunga, ili waweze kuazalisha zaidi, huku wakiwa na soko la uhakika.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, amewakaribisha wawekezaji katika Wilaya ya Ngara, huku akidai kwamba ni matumaini yake kuwa wataendelea kuja ngara, ili kuhakikisha kwamba mkataba huo unatekelezwa kwa mafanikio ya wananchi wa wilaya ya Ngara.
Amewashukuru muwekezaji na wabia wake, pamoja na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, ambao ni wawakirishi wa wananchi, kwa kukubali kusaini mkataba huo.
“Nasema mkataba huu ukitekelezwa na malengo yake yakatimizwa kama yalivyokusudiwa, utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wetu, kwanza kutoa ajira kwa watu 2500, si haba.” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Ngara.
Aidha, amefafanua kwamba wenyeji wanaozunguka mradi huo, watajifunza utaalamu mpya wa kuzalisha mazao ya biashahara kama vile kahawa, mpunga na avocado na kusaidia kutoa mbegu bora za mazao hayo kwa wananchi wa wilaya ya Ngara.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa