- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Wazazi na walezi wa watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wanachangia kuongezeka kwa wavivu na wazembe kutokana na malezi yao mabaya.” Alisema Paroko wa parokia ya Ngara Mjini Padre Sixmund Nyabenda wakati wa ibada ya Mei 01, 2018 ambayo ni siku ya Mt. Yosefu Mfanyakazi.
Paroko Nyabenda amesema wachapakazi katika kizazi hiki wanazidi kuwa bidhaa hadimu; iwe nymbani, maofisini na hata shambani, kwani vijana wengi wamekuwa watepetevu na akadi kuwa wamekuwa wazembe kiasi kwamba kila wanachotumwa wanalalamika.
“Watoto hawafanyi shughuli yoyote ile, kwani wakiamuka asubuhi wanakwenda shuleni, wakitoka shuleni wanakwenda ‘tuition’ wakirudi nyumbani wanakula na baada ya chakula cha jioni wanaangalia televisheni hawana nafasi ya kufanyakazi.” Alisema Baba Paroko Nyabenda.
Amesema hata Adamu alipoumbwa Mwenyezi Mungu alimpa bustani ya Edeni na sharti alilompewa ni kuitunza Bustani hiyo, na kuongeza kuwa kadiri ya maandiko matakatifu hata Mwenyezi Mungu, alifanyakazi na siku ya saba alipumuzika.
Uvivu na uzembe ni dhambi, na kuwataka waamini wafanye kazi kwa wakati uliopangwa na kwamba kazi inapofanywa kwa bidii na utaratibu uliowekwa; Mwenyezi Mungu anaibariki.
Aidha, amewataka vijana kutuliza akili akidai kuwa vijana wa sasa wamepoteza umakini na umaarufu wa kufanyakazi, kwa sababu ya kutotuliza akili zao na kuwa na tamaa mbaya.
Amewahasa kwamba mafanikio ya ndoto zao ni matoke ya bidii ya kufanyakazi sasa kwani maandiko matakatifu yanasema kwamba kama bawaba zikaavyo katika mlango kadhalika mvivu ukaa katika kitanda chake (Methali 26:14).
Siku ya Mei mosi ambayo pia ni sikukuu ya Mtakatifu Yosefu mfanyakazi, utumika kavibabriki vifaa vya kufanyia kazi halali, ambapo Baba Paroko Nyabenda alivibariki vifaa wanavyotumia waamini kufanyiakazi halali.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa