- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amewataka Mameneja wa Mikoa wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kuhakikisha wanaendelea na Mapambano dhidi ya rushwa katika maeneo yao ya kazi na nje ya kazi ili kujenga taswira nzuri kwa Wakala huo na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha Mamemeja hao, tarehe 17 Novemba, jijini Dodoma, Waziri Bashungwa amesisitiza Mameneja hao kuendelea na Mapambano dhidi ya Rushwa bila kuchoka kwenye sekta ya ujenzi kuanzia manunuzi na usimamizi wa miradi ya ujenzi.
Mhe Bashungwa amewata kuhakikisha kuwa wanaripoti kwake au katika mamlaka husika endapo watahisi kuna viashiria vyovyote vya Rushwa mapema ili hatua stahiki kuchukuliwa kwa wakati.
"Ninyi ni sehemu ya ulinzi wa kusaidia kupambana na Rushwa, msisite kuendelea kupambana na suala hili kwa pamoja kuanzia katika hatua za manunuzi hadi kwenye utekelezaji wa Mikataba, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kuona mnafanya weledi.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa