- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa kuandaa Mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Mikoa sambamba na makongamano ya vijana ili wabaini fursa zilizopo kwenye Mikoa yao.
Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo ya Uongozi kwa Viongozi wa Mkoa wa Kagera, ukumbi wa ELCT Bukoba Hotel, Mhe. Majaliwa ameeleza kuwa Mhe. Dkt. Philipo Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati ufunguzi wa Kongamano la Vijana wa Mkoa wa Dodoma alitoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa wote kuandaa makongamano ya Vijana ili vijana wakutane wabainishiwe fursa na wafundishwe namna ya kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao
"Nami niungane na Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwataka Wakuu wa Mikoa kuandaa mafunzo haya kama yalivyofanywa leo hapa Kagera kwa watendaji wetu ndani ya Serikali pamoja na kongamano la vijana ikiunganishwa nguvu ya pamoja Mkoa utaenda kwa kasi sana,"ameeleza Mhe. Majaliwa
Pia Mhe. Majaliwa ameainisha maeneo yenye msisitizo ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kufanya tathmini ili kubaini matokeo ya mafunzo hayo,kuwatumikia zaidi wananchi,kuwafuata na kutatua kero zao kuwasikiliza na kupata ufumbuzi wa kero zao hususani kero za ardhi,wafugaji na wakulima
Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa kuweka mikataba ya utendaji kazi na wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri zote, viongozi na watumishi kwenda kufanya kazi kwa weledi, kuwa waadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa
Ameendelea kueleza kuwa ni matarajio yake kwa muda ambao utakuwa umepangwa wa kutathmini matokeo ya mafunzo hayo ni vema kiongozi mwandamizi wa Taasisi ya Uongozi kuja kusikia kuona matokeo ya semina yake
Akitoa maelezo mafupi juu ya mwelekeo wa Mkoa wa Kagera baada ya Mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea watanzania maendeleo ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/24 Mkoa wa Kagera umepokea takribani ya Tsh. bilioni 281.3 ambazo zimepokelewa Halmashauri na Sekretarieti ya Mkoa, TARURA, TANROAD, RUWASA, TANESCO na REA.
Amebainisha changamoto zinazokabili Mkoa wa Kagera ni pamoja na kushuka kwa hali uchumi wa Mkoa wa Kagera ambao upo Mkoa upo nafasi ya 25, asilimia 34.5 ya watu wana udumavu na utapia mlo na mdondoko wa wanafunzi wanaoacha masomo ambapo takwimu za wanaocha masomo ni takribani wanafunzi elfu 16,726 kwa shule za msingi na 6,795 kwa shule za sekondari.
Hivyo kupitia mafunzo hayo viongozi wamejipanga na kuweka mkakati ili kuhakikisha changamoto zinatatuliwa na kuinua hali ya uchumi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa