- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri mwenye dhamana ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (Mb) amezindua Programu ya Kuinua Uchumi kupitia Ufugaji ijulikanayo kama "Kopa Ng'ombe Lipa Maziwa" inayotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Heifer International Kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania TADB, chini ya mradi wa kuboresha Sekta ya Maziwa (TI3P) kwa Kanda ya Ziwa na Zanzibar unaofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates (BMGF).
Waziri Ulega akiambatana na Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwasa wamefika Wilayani Karagwe Oktoba 03, 2023 na kuzindua mpango huo wa Kopa Ng'ombe Lipa Maziwa unaoratibiwa na Ndg. Jossam Ntangeki Mmiliki na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uchakataji Maziwa Cha Kahama fresh Ltd kilichopo Kihanga Karagwe.
Waziri Ulega amempongeza Ndg. Jossam kwa Kuuunga Mkono Kampeni ya BBT kwa Kuinua Vijana Kiuchumi, ukiwa ni mpango wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutaka Vijana wajiimarishe Kiuchumi kupitia Kilimo Uvuvi na Ufugaji wa Kisasa.
Awali akisoma Taarifa ya Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Kahama Fresh Bw. Jossam Ntangeki ambaye ni mmiliki wa kiwanda hicho ameitaja changamoto kubwa inayoukabili mradi wa Kahama Fresh kuwa ni upungufu wa sehemu ya malisho ya ng’ombe Ambao ndio chanzo cha maziwa ambayo ni malighafi ya kiwanda hicho
“Changamoto kubwa tuliyonayoni eneo la malisho,Mheshimwa Waziri tunashukuru kwa kipande kidogo tulichopewa ambacho ndiko tunafugia lakin hakitosh kabisa na tumeleta maombi yetu ofisini kwako na tunajua NARCO ni kampuni ambayo ipo chini yako Mheshimiwa Waziri na tumepeleka maombi yetu mda mrefu tu tukiomba tupatiwe eneo ambalo tutaweza kuweka shamba la kufugia Mitamba, kwa nafasi hii tunaomba ikikupendeza useme neno” amesema Bw.Ntangeki
Naye Waziri Ulega amemuhaidi Bwana Ntangeki kuwa ombi hilo atalifanyikia kazi mara moja na kumtaka kuwa ajiandae kupata eneo hilo maana amekuwa mfano wa kuigwa na kuongeza kuwa hata akipewa eneo hilo litatumika ipasavyo kwakuwa tayari ameshaonyesha njia na itafanya uzalishaji uongezeke na kuliongezea taifa kipato.
www.ngardc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa