- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakuu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wametakiwa kuweka mikakati ya kupunguza utoro wa wanafunzi ili kuinua kiwango cha kufaulu wilayani humo.
Haya yamesemwa na Afisa Elimu Takwimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Zacharia Mkumbo, wakati wa kikao kazi cha walimu wakuu wa shule za sekondari, kilichoandaliwa na Idara ya Elimu Sekondari kilichofanyika shule ya sekondari Ngara Julai 12, 2018.
“Kama wakuu wa shule tujiwekee mkakati wa kukomesha utoro ili takwimu za kufikia machi mwaka kesho zishuke, kwa sababu hadi sasa kila mmoja wetu anajua yuko wapi na anatakiwa kufanya nini ili kutimiza azma hiyo.” Alisema Ndugu Mkumbo.
Shule zinazoongoza kwa utoro ni Bukiriro yenye watoro 112, Shunga wanafunzi 80, Kibogora wanafunzi 58, Muganza wanafunzi 57, shule nyingine ni Rusumo yenye wanafunzi 52.
Amewataka wakuu hao wa shule kuwahimiza walimu wa madarasa, kuripoti na kuwafuatilia wanafunzi watoro na kuwarejesha shuleni, ili wasipoteze na kukosa haki yao ya msingi ambayo ni elimu.
Ndugu Mkumbo amesema walimu wa madarasa ni zaidi ya wazazi kwani wana muda mrefu wa kukaa na wanafunzi; hivyo wanawajibika kuhakikisha wanafunzi wote wanahudhuria shuleni hadi watakapohitimu masomo yao.
Naye Kaimu afisaelimu sekondari Ndugu Marton James amewakumbusha walimu wakuu wakomeshe tabia ya baadhi ya walimu shuleni kwao, wenye tabia ya kuwatukana watoto kwa madai kwamba tabia hiyo inawakatisha tamaa wanafunzi.
Amesema kwamba walimu wenye tabia hiyo wanaweza kuwa ndio chanzo cha uturo uliokithiri wa wanafunzi kwani hadi Machi 2018, wanafunzi wapatao 674 wameacha shuleni na kutokomea kusikojulikana.
Afisaelimu taaluma amewasisitiza wakuu hao kuwakumbusha walimu wao kujaza nyaraka muhimu za kufundishia zikiwemo adalio la somo, kujaza shajala za masomo pamoja na kuita majina kila siku ili kubaini wasiohudhuria shule.
Walimu wa kuu wameishukuru ofisi ya elimu sekondari kwa kuandaa kikao hicho ambacho kwao kimekuwa cha manufaa kwani wameweza kushirikishana kimawazo; huku wakikemea pale pasiponyooka.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa