- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya Ngara, wametakiwa kuwekeza katika elimu, kwa madai kwamba wapende wasipende wakati ni ukuta elimu tunakoelekea haikwepeki.
Ujumbe huo umetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Baragondoza, wakati akifafanua umuhimu wa Elimu ya Malezi (Day Care) kwa wazazi wa watoto, waliotimiza mwaka mmoja katika kituo cha J & J Patmos Center wilayani Ngara.
“Tunakokwenda ni kugumu sana kwa sababu vitu vingi viko kimtandao zaidi, kila unachokitaka lazima uingie kwenye mtandao, kwa hiyo tunataka hatutaki, tunapenda hatupendi; lazima tuwekeze kwenye elimu.” alisema Ndugu Baragondoza.
Amefafanua kwamba kuna tofauti kati ya Elimu ya Malezi na elimu ya awali yaani Chekechea, ambapo amesema watoto wa elimu ya malezi, wana umri wa kuanzia miaka mitatno kwenda chini, na wako chini ya usimamizi wa ofisi ya Ustawi wa jamii.
Watu wengi wamekuwa wakishindwa kutofautisha dhana hizi mbili hivyo, kuleta sintofahamu mablimbali, huku akisistiza kwamba kazi ya vituo hivi ni kuhakikisha watoto, wanaandaliwa kisaikolojia, kimakuzi, kimalezi na kihisia, ili wakue katika tabia nzuri.
Aidha, amesema vitu vinavyozingatiwa katika vituo hivyo vya elimu ya malezi; ni kuwalea watoto wakue kimichezo, na kufahamiana wao kwa wao, huku wakielekezwa katika mambo yatakayowasaidia kielimu pindi watakapoanza elimu yao ya msingi.
Wazazi wengi wamewekeza katika malenzi, ambayo yanaawanyima fursa watoto kukua kiakili, badala yake wanawakuza watoto wao kimwili; kwa maana ya kuwapatia chakula; lakini wanawanyima nafasi ya kutosha kuruhusu vipaji vyao kimakuzi.
“Vituo hivi serikali iliviruhusu, ili watoto wapate mahala pazuri pakupata mafunzo mazuri, kufahamiana na kukuza vipaji vyao; hilo ndilo lengo kubwa la kuanzisha Elimu ya Malezi hapa nchini.” Alisistiza Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya Ndugu Baragondoza.
Amewataka walezi waliopewa dhamana ya kuwalea watoto hao, kuwaangalia kwa makini, ili waweze kutambua vipaji vyao, na kuwaelekeza katika matamanio yao ya baadae, ili wawatengenezee njia njema kwa manufaa ya watoto hao na taifa kwa ujumla wake.
Naye Mgeni rasmi katika Hafla hiyo Ndugu Hissa Sama, amewaomba wazazi kutokuwa waonga kuwaandikisha wao katika shule hizi, bali wawapeleke katika vituo hivyo, ili waweze kupata mafunzo, ambayo ameyaita ni ya msingi katika makuzi yao.
“Msiogope kuwaandikisha watoto katika vituo vya elimu ya Malezi, kwa madai kwamba wataumia au watapata shida mbalimbali, shida hizo wanaweza kuzipata hata wakiwa nyumbani, watoto hao ni mali ya Mwenyezi Mungu na ndiye anayewalinda.” alisema Ndugu Sama.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa