- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lt Kanali Michael M. Mntenjele akiwaasa wanakamakti wa Afya juu ya Uhamasishaji wa Elimu ya Ebola
Afisa Afya Wilaya ya Ngara,Ndugu Salum R. Kimbau
Wanakamati wa Afya wilaya ya Ngara waliohudhuria kikao kuhusu ugonjwa wa Ebola,Ngara
WILAYA YA NGARA YAANZA KUCHUKUA TAHADHALI JUU YA UGONJWA WA EBOLA
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi za Uganda na Congo, wilaya ya Ngara imeanza kuchukua tahadhari kwa kutoa elimu kwa wananchi wa vijiji vinavyopakana na nchi za jirani, pia imejenga vituo na kusambaza vifaa vya kupimia wageni waingia nchini. Vituo hivyo vimejengwa katika Kata za Rusumo, Kabanga na Murusagamba.
Akizungumza katika kikao kilichofanywa tarehe 21 Juni 2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kilichokuwa na agenda kuu ya Ugonjwa wa Ebola, Afisa Afya Wilaya ya Ngara Ndugu Salum R. Kimbau amesema wilaya imetenga kituo cha Afya cha Lukole maalum kama kambi ya kuhudumia wagonjwa watakaobainika kuwa na maambukizi ya Ebola.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Luteni kanali Michael M. Mtenjele ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho aliwasisitiza wajumbe wa kamati ya Uhamasishaji kutoa elimu kwa wananchi hasa wa vijiji vilivyo karibu na mipaka ya nchi jirani kutoruhusu au kupokea wageni kutoka nchi jirani wanaotumia mipaka isio rasmi kuingia nchini. Pia aliwaomba vyombo vya Usalama kusaidia kudhibiti wageni watakaoingia nchini bila kufuata taratibu za kisheria.
“Kujihami ni suala la ushirikiano , maana kutojali kwa raia mmoja kutasababisha madhara kwa jamii kubwa,hivyo wananchi waache mazoea ya kupokea wageni wan chi jirani waingiao kienyeji na waripoti mara moja pale waonapo mgeni aliyeingia kwa njia zisizo rasmi”,alimalizia Mkuu wa Wilaya ya Ngara.
Wahamasishaji katika kikao hicho wameombwa kushirikiana na taasisi za dini katika kutoa elimu juu ya ugonjwa huo na pia kuwaelimisha waumini wao juu ya tahadhali za kuchukua ili kuepuka ugonjwa huo kuingia nchini.
Mpaka sasa takwimu zinaonesha kuwa hakuna mtu aliyepatikana na ugonjwa huo katika nchi ya Tanzania na hivyo ni jukumu letu kuendelea kuelimishana sisi kwa sisi ili kwa pamoja tuweze kuepuka ugonjwa hatari wa Ebola.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa