- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoa wa kagera imepeleka Mkimbiaji Bi Leah N Emmanuely ambaye alishiriki Mashindano ya watumishi Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) Jijini Dodoma na kufanya vizuri kitaifa katika Mbio fupi Mita 100, 200 na 400. Kwa kushika nafasi za 2 na 3 kitaifa.
Mkimbiaji huyo ni mmoja wa wakilishi Mkoa wa kagera akitokea wilayani Ngara.
Mashindano ya Riadha Kwa wanawake "ladies first" yameandaliwa na Baraza la michezo la Taifa (BMT) Kwa kushirikiana naTasisi ya Ushirikiano wa kimataifa ya Japani.
Mashindano hayo Yanalenga kuandaa timu ya taifa ya wanawake itakayoshiriki katika Mbio kimataifa.
Mbio zitakazoshindaniwa ni fupi na Ndefu, Mbio hizo ni Mita 100, 200,400,800,1500,5000, na 10,000.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngara wakati wa kumuaga Mwanamichezo huyo alimtakia mashindano mema Kwa kweda atakuwa ameitangaza Wilaya ya Ngara pia Mkoa wa kagera kupitia michezo.
Afisa utumishi Ndg Bahati Marco akiwa uwanja wa taifa na mwanariadha kutoka Ngara na Bukoba wanaouwakilisha Mkoa wa kagera
Wanariadha wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi katibu wa BMT Bi Neema Msita, M/kiti BMT Tenga na Katibu mkuu wizara ya Utamaduni sanaa na Michezo Ndg.Greyson Msigwa uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa