- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Wahandisi ambao wana uwezo wa kufanyakazi tutawapa ushirikiano, wahandisi wababaishaji hawana nafasi ya kufanyakazi katika wakala wa maji vijijini; kwa sababu tumejipanga kuhakikisha adhima yetu ya kumtoa mwanamama ndoo kichwani inakamilika.” Alisema Naibu Waziri wa Maji Mh. Jumaa Hamidu Aweso.
Naibu waziri wa Maji Mh. Aweso ameyasema hayo Januari 13, 2019 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wakati wa ziara yake ya siku moja Wilayani humo, ambapo amesema waliagizwa kuhakikisha watanzania wanapata maji safi, salama na yenye kutoshereza.
Maji hayapatikani kwa kukaa ofisini na kuzunguka kwenye kiti cha kuzunguka; maji yanapatikana kwa wataalamu kwenda vijiijini kuona maedeleo ya miradi ya maji inavyotekelezwa, na inapokwama hasa changamoto zinazowakabiri wananchi.” Alisema Mh. Aweso
Zipo jitiada zinazofanywa na serikali kutatua matatizo ya upatikanaji wa maji; kwa mfano, Bukoba kuna mradi mkubwa ambao serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni 31; lakini yapo maeneo ya pembezoni hayana maji kama Ihungo.
Amsema Wizara inatoa nguvu kwa Manispaa ya Mji wa Bukoba, ili kuhakikisha kwamba maeneo ya pembezoni nayo, yanapata maji, ili wananchi wa mjini humo waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Kubwa alilogundua katika Mkoa wa Kagera ipo miradi mikubwa imekamilika, lakini haitoi maji; mingine iliyokamilika matenki yanavujua na imetelekezwa na wakandarasi wamelipwa fedha lakini wananchi hawapati huduma ya maji.
“Unamlipaje mkandarasi kazi hajaifanya vizuri, na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake; sisi kama wizara ya maji hakuna mhandisi yeyote, ambaye ataaribu miradi ya maji halafu ategemee sisi tutamhamisha; tutamchukulia hatua na kama ameshiriki na wakandarasi kula fedha za serikali ajiandae kuzitapika.” Alisistiza Waziri Aweso.
Kwa hiyo Wizara imeanzisha wakala wa maji vijijini na mswada umeishasomwa bungeni, ambao baadae wanatarajia uatapita Bungeni ili uwe sheria kusidi Wizara iweze kuchukua hatua stahiki kwa wabadhirifu wa miradi ya maji.
Amesema kabla hao wahandisi wa maji hawajanza kufanya kazi na wakala wa huduma ya maji vijijini, watapigwa msasa kwa sababu watakaosimamia wakala huu ni hao hao waandisi, ambao wanatoka katika Halmashauri za wilaya.
Amekiri kuwepo kwa changamoto ya ucheleweshaji wa fedha za miradi, na kuahidi kuyalipa madeni ya wakandarasi wa maji hapa Wilayani Ngara; ambapo kiasi wanachodai amekitaja kuwa ni kama shilingi milioni 231,000,000
Naye Kaimu Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Eng. Simon Ndymukama amekiri kuwa Mji wa Ngara una upungufu mkubwa wa maji kwa sababu ya changamoto tau meme na ongezeko la watu.
“Ni kweli maji yanapatikana kwa mgao; ambapo maeneo mengine wanapata maji mara mbili kwa wiki; lakini wengine inaweza ikawa mara moja kwa wiki, tatizo kubwa ni changamoto ya umeme, kwani ni mdogo kuweza kuendesha mitambo ya kusukuma maji.” Alisema Eng. Ndyamukama.
Pia maji yanayozalishwa ni kidogo ikilinganishwa na uhalisia na kudai kwamba mfumo wa maji uliopo umejengwa mwaka 1972 na ongezeko linakuwa wahitaji huduma eneo la mjini; huku miundombinu ni ile ile.
Hata hivyo, amesema kuna mradi mkubwa wa miji sita ambapo Ngara ni miongoni mwa wilaya zitakazinufaika na mradi huo, na uko katika hatua za mwisho za kuanza; utakapokamilika tatizo la maji katika mji wa Ngara utakuwa ndo mwisho wake.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa