- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera shilingi milioni 800, kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya huduma za afya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ndugu Erick Nkilamachumu, alisema hayo Machi 26, 2018, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa miundombinu katika vituo vya afya vya Mabawe na Murusagamba.
“Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 400, zinatumika kituo Afya cha Mabawe na nyingine zinatumika katika kituo cha afya cha Murusagamba, kwa ajili ya kujenga majengo ya upasuaji, wodi za wagonjwa, nyumba za waganga na maabara.” Alifafanua ndugu Nkilamachumu.
Ameitaka kamati ya ujenzi ya kata ya Mabawe kuacha malumbano, bali wafanye kazi na vikao vya maamuzi kwa kuwashirikisha wananchi, ili waweze kusogeza vifaa vinavyohitajika.
“Haiwezekani serikali itume fedha za kuboresha huduma za matibabu, viongozi wa kamati muanzishe malumbano; tafadhali kila kitengo kisimamie majukumu yake” Alisema Nkilamachumu
Aliwashauri wananchi kuchangia 15,000/= kila kaya kwa ajili bima ya Afya, ili waweze kupata huduma ya matibabu kwa watu sita kwa mwaka mzima.
Wakati huo huo, Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya cha Murusagamba Dkt Godian Beyanga, amesema kwamba kituo chake kinahitaji umeme wa uhakika, kwani wanaotumia ni wa nguvu za jua, wakati wa mvua unakuwa ni hafifu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa