- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mnamo tarehe 12 Februari, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilipata ugeni kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii,jinsia, Wazee na Watoto ambapo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula aliongoza msafara huo.
Wakati wa ziara hiyo Dkt. Chaula alifanya ukaguzi wa mpaka wa Rusumo jengo la OSBP kuangalia namna Halmashauri ya Wilaya Ngara ilivyojiandaa kujikinga na kuzuia magonjwa ya mlipuko yasiingie nchini. Dkt Chaula alizihakiki hatua na vifaa vitumikavyo kumpima mtu aingiapo nchini ambapo alisisitiza Wataalam kuwa makini na kuzingatia mafunzo na maelekezo yaliyotolewa na Wizara juu ya upimaji ili kuimarisha ufuatiliaji wa wasafiri hasa waingiao nchini kupitia mpaka huo na mipaka mingine.
Pia, Dkt. Chaula aliupongeza uongozi wa Halmashauri na OSBP kwa hatua na juhudi wanazofanya katika kuhakikisha magonjwa hayo hatarishi ya Ebola na Corona hayaingii nchini. Dkt chaula alisema ”Juhudi zilizofanywa na serikali katika kupambana na magonjwa haya kuingia nchini ni kubwa mno,hivyo niwapongeze Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa juhudi na utekelezaji mzuri mnaoufanya katika mipaka na wilaya nzima kwa ujumla”.
Aidha, Dkt Chaula aliomba Halmashauri kuboresha mazingira ya “Holding Center” kwa kuwa na choo maalum kwa washukiwa ,kutoa elimu ya unawaji mikono kabla ya kuingia chumba cha kupimia joto na pia kuangalia namna ya kupunguza uwezekano wa watu kugusana au kugusa vitu kwa pamoja.
Mwisho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ngara Ndugu Sangatati T. alimshukuru Katibu Mkuu kwa ujio wake katika Halmashauri ya Ngara na pia alimuahidi kuyafanyia kazi maboresho yaliyopendekezwa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia, Wazee na Watoto.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa